Mkuu wa Wilaya ya Wanging'ombe Comrade Bro Ally Kasinge anawatangazia wananchi wote wa Wilaya ya wanging'ombe kuwa Mwenge wa Uhuru utakimbizwa Wilayani tarehe 16/09/2019, ukiwa Wilayani Mwenge wa uhuru utakagua,kuzindua na kuweka mawe ya Msingi kwenye miradi mbalimbali ndani ya Wilaya, aidha Mwenge huo utapokelewa kijiji cha Wanging'ombe katika viwanja vya shule ya Sekondari Wanging'ombe ukitokea Halmashauri ya Mji Makambako, Mwenge wa uhuru utapita katika vijiji vifuatavyo Wanging'ombe,Litundu,Mayale,Ilembula,Luduga,Mambegu,Mtapa, Chalowe na Kukesha katika viwanja vya Soko katika Kijiji cha Igwachanya,Mkuu wa Wilaya anawaomba wananchi kujitokeza katika kuulaki Mwenge wa Uhuru kwenye maeneo yote utakakopita na kukesha."Amani Mshikamano na Maendeleo"
Copyright ©2021 Wanging'ombedc . All rights reserved.