IDARA YA ARDHI NA MALIASILI
Utangulizi
Idara ya Ardhi na Maliasili inaundwa na Sekta ya Ardhi na Maliasili, ikiwa na jumla ya vitengo saba (7) ambapo Sekta ya Ardhi ina jumla ya vitengo vinne (Ardhi, Mipangomiji, Upimaji na Ramani pamoja na Uthamini) na Sekta ya Maliasili ina jumla ya vitengo vitatu (Misitu, Wanyama Pori na Utalii).
Taarifa za Watumishi
Idara ina jumla ya watumishi saba (7).
Sekta ndani ya Idara na shughuli zake
Sekta ya Ardhi na Majukumu ya kila Kitengo
Kitengo cha Mipangomiji
Kuandaa mipango ya maeneo yaliyoendelezwa kiholela
Kuhuisha ramani za msingi kwa kushirikiana na kitengo cha Upimaji na ramani
Kutayarisha michoro ya mipangomiji
Kutayarisha mipango ya matumizi bora ya ardhi ya vijiji
Kuratibu utekelezaji ya michoro ya mipangomiji iliyobuniwa
Kuchambua, kukagua na kutoa mapendekezo yanayohusu mabadiliko ya matumizi ya ardhi na umegaji wa viwanja
Kupitia na kufanyia marekebisho michoro ya mipangomiji
Kuhakiki mapendekezo ya mipango kama yanakidhi haja za kimazingira (Environmental Impact Assessment)
Kushughulikia maombi ya mabadiliko ya matumizi ya ardhi
Kupokea na kushughulikia migogoro inayohusiana na matumizi ya ardhi
Kutoa mapendekezo ya masharti ya uendelezaji wa ardhi
Kutambua na kukagua maeneo yenye athari za kimazingira (hazardous lands)
Kukagua na kupitisha ramani kwa ajili ya vibali vya ujenzi
Kutoa elimu kuhusiana na masuala ya mipangomiji na vijiji
Kitengo cha Upimaji na Ramani
Kufanya upimaji wa viwanja kulingana na michoro ya mipangomiji iliyoidhinishwa
Kufanya upimaji wa mashamba
Kukagua kazi za upimaji na kuziwasilisha kwa Mkurugenzi wa Upimaji na Ramani
Kupokea na kushughulikia migogoro ya mipaka ya mashamba na viwanja
Kurudishia alama za upimaji inapohitajika
Kutoa elimu kuhusiana na masuala ya upimaji na ramani
Kuhakiki na kutunza kumbukumbu za upimaji miliki (cadastral database)
Kushauri Halmashauri kuhusu masuala ya Upimaji na utayarishaji wa ramani
Kitengo cha Uthamini
Kupokea maombi ya kufanya uthamini
Kukagua, kupima na kuanisha thamani ya majengo na ardhi kwa ajili ya kumbukumbu (data bank)
Kufanya uthamini kwa madhumuni mbalimbali (malipo ya fidia, kodi za nyumba, rehani, bima, mizania (balance sheet) na mauzo ya mali)
Kusimamia, kuhakiki na kudhibiti uandaaji wa kumbukumbu zinazohusu utekelezaji na mwenendo wa soko la ardhi
Kusimamia utekelezaji wa miongozo na sera za serikali
Kukagua taarifa za uthamini wa serikali na makampuni binafsi na kuwasilisha mapendekezo kwa Mthhamini Mkuu wa Serikali kwa ajili ya kupitishwa
Kufanya uthamini wa mali zinazokutwa katika eneo la mpango
Kukokotoa na kutayarisha taarifa za uthamini
Kutoa elimu kuhusiana na masuala ya Uthamini
Kitengo cha Ardhi
Kuingiza kumbukumbu katika komputa
Kutoa ushauri kwa wateja
Kushughulikia utayarishaji wa nyaraka za kisheria
Kufanya ukaguzi wa viwanja
Kutoa notisi na kupendekeza ubatilishaji wa miliki kwa viwanja visivyoendelezwa kwa mujibu wa sheria
Kuwasiliana na wateja kuhusu hati zilizotayarishwa na kuwakabidhi
Kutoa ushauri na mapendekezo ya utoaji upya miliki na ulipaji fidia za ardhi
Kutoa ushauri wa ugawaji wa viwanja na mashamba makubwa zaidi ya ekari 500
Kuchambua migogoro ya ardhi na kutoa ushauri
Kudhibiti masharti ya uendelezaji ardhi
Kuratibu masuala ya Ardhi juu ya elimu kwa umma
Copyright ©2021 Wanging'ombedc . All rights reserved.