KITENGO CHA MANUNUZI
Kitengo cha Manunuzi Katika Halmashauri ya Wilaya ya Wanging’ombe kilianzishwa kwa mujibu wa Sheria ya Manunuzi Na. 07 ya mwaka 2011 kifungu cha 37.
Kitengo cha Manunuzi katika Halmashauri ya Wilaya ya Wanging’ombe kina Watumishi 3 wapo makao makuu
Mfumo wa mawasiliano kwa mujibu wa sheria ni kuripoti moja kwa moja kwa Mkurugenzi, pia kitengo kina bajeti inayojitegemea ili kutekeleza majukumu yake.
Majukumu ya Kitengo cha Manunuzi.
Kusimamia majukumu yote ya Manunuzi na Kuuza Mali za Halmashauri.
Kusaidia kazi za Bodi ya zabuni.
Kutekeleza Maamuzi ya Bodi ya Zabuni.
Kuandaa Mpango wa manunuzi wa Halmashauri na uuzaji wa Mali za H/W.
Kushauri Manunuzi ya H/W na uuzaji wa Mali za H/W.
Kuandaa orodha ya mahitaji ya Idara na Vitengo.
Kuandaa Makabrasha ya Zabuni.
Kuandaa Matangazo ya Zabuni na Fursa Mbalimbali.
Kuandaa Mikataba mbalimbali ya manunuzi.
Kutoa makabrasha ya mikataba ambayo imepitishwa na
Kutunza kumbukumbu mbalimbali za manunuzi na uuzaji wa mali za H/W.
Kuandaa orodha ya mikataba yote ambayo H/W imeingia na wazabuni.
Kuandaa taarifa za mwezi, robo na mwaka za Bodi ya zabuni ya H/W.
Kuandaa Taarifa za Robo na kuwasilishwa katika vikao vya Kamati ya Fedha Mipango na Utawala.
Kuratibu manunuzi na uuzaji mali za H/W.
Kuandaa Taarifa nyingine mbalimbali kadri zinavyohitajika na Mamlaka.
Copyright ©2021 Wanging'ombedc . All rights reserved.