Taasisi ya fedha (CRDB Benki) imekabidhi Madawati 50 Shule mpya ya Sekondari Mtapa ikiwa na lengo la uboreshaji miundombinu ya elimu.
Akiongea baada ya Makabidhiano ya Madawati hayo, Meneja Mahusiano biashara za Serikali Nyanda za juu Bi. Paschalina Diu amesema Sekta ya elimu inahitaji miundombinu bora na ya kisasa ambayo itamfanya mwanafunzi kupata mazingira rafiki ya kusoma kwa bidii asome kwa bidii na kutengeneza mazingira rafiki ya kujisomea na tunatarajia kuendelea kuwezesha samani hizi kwa shule nyinginezo na itakuwa programu endelevu.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Wanging'ombe Dkt.Peter Maiga Nyanja ametoa shukrani za dhati kwa CRDB Benki ambapo ameonyesha kutambua mchango wao katika sekta za Elimu, Afya, Maendeleo ya Jamii na Kilimo.
Pia Dkt. Nyanja ameendelea kwa kuipongeza Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa utekelezaji wa Mradi wa Ujenzi wa shule za Msingi na Sekondari katika Wilaya ya Wanging'ombe ambapo vimechangia kuongeza mwamko wa Elimu bora katika Wilaya ya Wanging'ombe.
Baadhi ya Wananchi wamehudhuria hafla hiyo ya makabidhiano ya Madawati, wakiwakilishwa na Diwani wa Kata ya Igwachanya, Mhe. Anthony Mawata amesema kupitia madawati hayo wanategemea mazingira ya kusoma kwa wanafunzi hao yameboreka hivyo tunatarajia matokeo mazuri na ya ufaulu kwa wanafunzi.