Wilaya ya Wanging’ombe ni miongoni mwa Wilaya za Mkoa wa Njombe.Ilianzishwa mwezi machi 2012 kabla hapo ilikuwa sehemu ya Wilaya ya njombe vijijini. Jina Wanging’ombe limetokana na jina la kijiji cha Wanging’ombe ambacho kipo katika kata ya Wanging’ombe. Makao makuu ya Wilaya ya Wanging’ombe yapo kijiji cha Igwachanya katika kata ya Igwachanya.
Wilaya ya wanging’ombe ina ukubwa wa eneo lenye Kilomita za Mraba 3440.54, ikiwa na watu 161816 kwa mujibu wa sensa ya mwaka 2012. Wakazi wa wilaya ya Wanging’ombe ni Wabena,wakinga,wahehe na watu wa kabila tofautitofauti.
Wilaya ya Wanging’ombe ina Tarafa 3,Kata 21 na Vijiji 108. Ikolojia ya Wilaya ya Wanging’ombe imegawanyika katika makundi mawili kuna maeneo ni ya ukanda wa baridi na ukanda wa joto.
Kutokana na ilkolojia hiyo wakazi wa Wanging’ombe wanajishughulisha na shughuli za kilimo cha mazao ya chakula ambayo ni mahindi, mtama, viazi mviringo,viazi vitamu, maharage, mihogo, njugu mawe, ngano, kunde na njegere na mazao ya biashara kama vile kahawa, chai, alizeti, pareto na karanga pamoja na Ufugaji.Pamoja na shughuli za kilimo wakazi wa wanging’ombe pia wanajishughulisha na ufugaji wa nyuki ,ufugaji wa Ng’ombe,Mbuzi,Kuku pamoja na biashara ndogondogo.
HISTORIA YA VIONGOZI WA WILAYA YA WANGING’OMBE
NA.
|
JINA KAMILI
|
MWAKA ALIONZA
|
MWAKA ALIONDOKA
|
1. |
Anthon Emmanuel Mahwata |
2013 |
- |
Copyright ©2021 Wanging'ombedc . All rights reserved.