IDARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII
Sehemu hii inajumuisha na hospitali ya Wilaya ya Wnging’ombe, lengo la sehemu hii ni kusaidia au kuwezesha utoaji wa huduma bora za Afya za kinga, matibabu na maendeleo ya huduma za Afya na Ustawi wa Jamii katika Wilaya. Seksheni hii inaongozwa na Mganga Mkuu wa Wilaya ambaye anawajibika kwa Mkurugenzi wa Wilaya.
Idara ndogo ndogo ndani ya Afya
• Elimu ya Afya
• Huduma za Tiba (Magonjwa ya ndani, Watoto, wajawazito, Upasuaji na Mifupa, Huduma za mionzi, Maabara na Mortuary)
• Huduma za Kinga (Huduma za Afya ya mama na mtoto na Huduma za kuzuia magonjwa ya kuambukiza)
• Utengemao (Rehabilitation)
• Ustawi wa Jamii
• Afya ya Mazingira
Majukumu ya Seksheni ya Afya na Ustawi wa Jamii
Majukumu ya Idara/Seksheni
Majukumu ya seksheni/sehemu ya Afya na Ustawi wa Jamii:
• Kuratibu na kushauri juu ya utekelezaji wa wa sera za Afya katika Wilaya
• Kuratibu masuala ya Afya na Ustawi wa Jamii katika Wilaya
• Kusimamia utoaji sahihi wa huduma za Afya zinazotolewa na hospitali/vituo vya Umma na sekta binafsi katika Wilaya
• Kuzijengea uwezo Hospitali, ZAhanati na vituo vya Afya katika utoaji wa huduma za Afya
• Kutoa ushauri wa kitaalamu katika uandaaji wa mipango ya upambanaji/uzuiaji wa tatizo la Virusi/UKIMWI (HIV/AIDS)
• kutoa ushauri wa kitaalamu juu ya uendeshaji wa shughuli zinazohusiana na masuala ya Virusi/UKIMWI (HIV/AIDS) katika Mkoa
• Kutoa huduma za Afya/msaada unaohitajika wakati wa milipuko ya magonjwa katika Mkoa
• Kutoa huduma za kliniki na matibabu kwa wagonjwa wa ndani na nje wanaoletwa kutoka vituo vya Afya/hospitali za mamlaka za serikali za mitaa
• Kutoa huduma za kitaalamu (utaalamu wa kubobea) za matibabu
• Kutoa/Kusaidia huduma za kitaalamu na msaada unaohitajika kwa vituo vya Afya na Hospitali za Mamlaka za Serikali za Mitaa wakati wa milipuko ya magonjwa yakuambukiza
• Kutoa huduma za rufaa za maabara na vipimo
• Kuratibu upatikanaji wa madawa/vifaa tiba kwa ajili ya hospitali
HALI YA AFYA NA USTAWI WA JAMII
Mafanikio yaliyopatikana katika Sekta ya Afya ni kama ifuatavyo:-
Vituo vya kutolea huduma.
• Mwaka 2013 Wilaya ina Hospitali 1, Vituo vya Afya 3 na Zahanati 37, Mwaka 2014 Wilaya ina jumla ya Hospitali 1, Vituo vya Afya 4 na Zahanati 40.
• Mgawanyo wa Huduma za Afya na wamiliki Mwaka 2017 ni kama ifuatavyo:
o HUDUMA ZA AFYA o MMILIKI
o WANGING’OMBE
o Zahanati • 1. Serikali o 39
• 2. Binafsi/Shirika o 1
• JUMLA 40
o Vituo vya Afya • 1. Serikali o 2
• 2. Binafsi o 2
• JUMLA o 4
o Hospitali • 1. Serikali o 0
• 2. Binafsi o 1
• JUMLA o 1
o JUMLA • 1. Serikali o 41
o JUMLA • 2. Binafsi o 4
• JUMLA o 45
Kwa kipindi hicho vituo vya kutolea huduma vimeongezeka kutoka 41mwaka 2013 hadi 45 mwaka 2014. Hii ni sawa na ongezeko la asilimia 63.
Huduma za Mama na Watoto
• Katika kipindi cha mwaka 2005 na 2014, idadi ya akina Mama wajawazito wanaojifungulia katika vituo vya kutoa huduma imeongezeka. Mwaka 2005 ilikuwa asilimia 56, kiwango kimeongezeka hadi kufikia asilimia 94 hadi kufikia Agosti, 2014.
• Kwa Mujibu wa taarifa ya Vifo vya watoto wachanga (Infants Kupunguza vifo vya wakinamama vinavyotokana na ujauzito kutoka 112/100,000 (2010), 65/100,000(2011) hadi 38/100,000 (Desemba 2012).
• Kupunguza vifo vya watoto chini ya mwaka mmoja kutoka 12/1000 (2010), 7/1000(2011) hadi 6/1000 (Desemba 2012).
• Idadi ya kaya zenye vyoo bora zimeongezeka kutoka 43% (2011) hadi 67%.(2012)
• Vifo vitokanavyo na ugonjwa Malaria vimepungua kutoka 21% (2011) hadi 18% (2012)
• Aidha, kiwango cha utoaji wa chanjo kwa watoto wenye umri chini ya mwaka mmoja kimeongezeka kutoka asilimia 87 kwa Mwaka 2005 hadi kufikia asilimia 92 Agosti, 2014.
Jitihada za Wilaya katika kupambana na maambukizi ya Virusi vya UKIMWI:
i) Kutoa elimu jinsi ya kujizuia na maambukizi ikiwa ni pamoja na Matumizi ya kondomu na kuwa na mpenzi mmoja.
ii) Kuendesha kampeni ya tohara kwa wanaume kupitia kampeni ya dondosha mkono sweta. Mwaka 2015 wamefanyiwa wanaume 2966 na mwaka 2016 mpaka mwezi Agosti wamefanyiwa 2285.
iii) Kuongeza vituo vinavyotoa huduma ya kuzuia maambukizi toka kwa mama kwenda kwa mtoto.
iv) Kuongeza idadi ya wagonjwa waliotambuliwa kuwa na Virusi vya UKIMWI kutumia dawa za kurefusha maisha (ARV)
v) Kutoa elimu ya Kujikinga na UKIMWI, kwa njia ya mikutano na sinema ,mila na desturi zinazochangia maambukizo ya VVU, kutoa elimu ya stadi za maisha na afya ya uzazi kwa Vijana na uundaji wa klabu za vijana katika vijiji.
vi) Kusaidia watoto yatima Sekondari na vikundi vya watu wanaoishi na virusi vya ukimwi

Copyright ©2021 Wanging'ombedc . All rights reserved.