UTANGULIZI
Idara ya kilimo, Umwagiliaji na Ushirika ni mojawapo ya Idara muhimu sana katika mamlaka ya serikali za mitaa Halmashauri ya wilaya ya Wanging’ombe.
Idara ina majukumu makubwa ya kusimamia na kufuatilia shughuli zote zihusuzo kilimo cha mazao ya aina zote yaani chakula na biashara, kusimamia masuala yote ya umwagiliaji na mambo ya ushirika katika eneo lote la Halmashauri ya Wilaya ya Wanging’ombe.
Idara ina vitengo vitatu tu yaani Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika.
MAJUKUMU YA IDARA
Kumshauri Mkurugenzi Mtendaji masuala yote yanayohusu Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
Kutoa miongozo, sera na kanuni za kilimo bora cha mazao ya aina zote
Kuratibu shughuli zote zinazohusiana na uendelezaji mazao
Kushauri na kusimamia shughuli zote za umwagiliaji kwa kushirikiana na wataalam kutoka tume ya umwagiliaji kanda na Taifa
Kuandaa taarifa za utekelezaji wa malengo yaliyopangwa na zinginezo na kuziwasilisha sehemu husika
Kutoa ushauri wa kitaalam juu ya uzalishaji wa mazao ya aina zote yanayostawi na yanayoweza kustawi katika Halmashauri ya Wilaya ya Wanging’ombe
Kuandaa, kuratibu na kupanga mipango ya maendeleo na bajeti ya idara ya kila mwaka, taarifa za utekelezaji na kuziwasilisha taarifa kama inavyotakiwa.
Kushirikiana na taasisi za utafiti na wadau wengine kufanya majaribio ya tekinolojia mbalimbali za kilimo.
Kuratibu watoa huduma wote wa sekta ya kilimo, umwagiliaji na ushirika
Kuhamasisha, kuunda na kusimamia uendeshaji wa vyama vya ushirika na vikundi vingine.
TAARIFA ZA UTEKELEZAJI
Taarifa za mwezi, robo mwaka, nusu mwaka na mwaka zinaandaliwa za mpango wa maendeleo ya kilimo za kijiji, kata na Halmashauri.
Taarifa zote za utekelezaji za watumishi wa idara wa Halmashauri na wadau wa sekta ya kilimo, umwagiliaji na ushirika zinaandaliwa na kuwasilishwa kwenye kamati za viongozi ndani ya Wilaya, mkoa na Taifa.
Taarifa za ufuatiliaji na tathimini zinaandaliwa. Miradi, Mvua, watumishi nk.
MASWALI MBALIMBALI YANAYOULIZWA NA WANANCHI
Ruzuku ya pembejeo zingine za mazao kama ilivyo kwa mbolea na mbegu za mahindi
Kuibuka kwa magonjwa yenye tabia mpya na sugu kutibika
Kuibuka tabia mpya za wadudu katika kushambulia mimea na usugu wao dhidi ya madawa
Bei kubwa ya pembejeo. Kwa sasa serikali imetoa bei elekezi ya DAP na UREA.
HATUA MBALIMBALI WANAZOTAKIWA KUFUATA KATIKA KUPATA HUDUMA
Kuwatumia (kwa karibu) wataalam wa ugani kilimo katika hatua zote za uzalishaji
Matumizi sahihi ya viuatilifu kwa kufuata vipimo sahihi, kiuatilifu sahihi, muda sahihi na kuvaa vifaa kinga
Wataalam kupata mafunzo mara kwa mara ili kuendana na wakati
Kutumia vema kanuni za kilimo bora
TAARIFA ZA MILIPUKO YA WADUDU NA MAGONJWA KUCHUKUA WANANCHI
Wadudu
Magonjwa
Sera inatambua misingi ya ushirika ya kimataifa ambayo ni;
Uanachama wa hiari
Demokrasia
Kujitegemea kiuchumi
Uhuru wa maamuzi
Elimu na mafunzo
Ushirikiano
Kujali Jamii.
“KUUNDA VYAMA VYA USHIRIKA IMARA NA ENDELEVU VYENYE UWEZO WA KUKIDHI MAHITAJI YA WANACHAMA YA KIUCHUMI NA KIJAMII”
Jukumu kuu la sera ni kuandikisha na kuendeleza vyama vya ushirika ambavyo ni:-
Msingi wake ni wanachama
Vinafanya shughuli zake kiushindani vikiwa vyombo huru vya kiuchumi
Vinawajali wanachama kwa ujumla wao
Vinafanya kazi kwa manufaa ya maendeleo ya kiuchumi na kiuchumi ya wanachama wenyewe na Jamii.
Inawapa wanachama uwezo na mwongozo wa kuweka mfumo unaokidhi mahitaji yao
Inatambua umuhimu wa kuwa na vyama vya Ushirika vya msingi na shirikisho
Inatambua kuwepo kwa vyama vya Ushirika vya kati na kilele kutegemeana na matakwa na maamuzi ya wanachama
Inaweka utaratibu wa uchaguzi wa viongozi na ajira kwa watendaji unaozingatia maadili ya uongozi
Inaelekeza uandikishaji wa vikundi vya kiuchumi vya wananchi kabla havijawa vyama vya Ushirika kamili
Inahimiza ukaguzi wa hesabu za vyama na utoaji taarifa
Kanuni za vyama vya Ushirika zinaelekeza jinsi utekelezaji wa sheria hiyo ya Ushirika kulingana na mchepuo.
Kuwezesha uandikishaji wa vikundi vya kiuchumi kuwa vyama vya Ushirika, kushauri kufuata na kusimamia vyama vya Ushirika.
Kusimamia utekelezaji wa sheria ya vyama vya Ushirika
Kufanya uchunguzi na ukaguzi kuhusu uendeshaji wa shughuli za Ushirika
Kujasirisha wanachama na viongozi kwa kuwawezesha kupata elimu na stadi za kuendeleza vyama vyao
Kutoa huduma za ushauri na kuweka mazingira muafaka yatakayowezesha ukuaji na uendelezaji wa Ushirika
Kuhakikisha kuwa kesi zinazohusisha vyama vya Ushirika zinashughulikiwa kwa haki.
USHIRIKA:
Ni muungano wa watu waliokubali kuendesha shughuli zao za Kiuchumi kwa pamoja na kuinua shughuli zao za maisha.
CHAMA CHA USHIRIKA:
Kwa mujibu wa Sheria ya Vyama vya Ushirika Na 20 ya Mwaka 2003,
Ni muungano wa watu ambao kwa hiari wameamua kujiunga kwa pamoja kuunda chombo kinachoongozwa kidemokrasia ambao huchangia kiasi kinachohitajika kufanya mtaji unaohitajika kuunda chombo hicho wanaokubali kupokea manufaa na hasara yatokanayo na shughuli za chombo hicho.
AINA:
Zipo aina nyingi kutegemeana na mahitaji mfano, SACCOS, AMCOS n.k. Idadi ya wanachama hutegemea shughuli ya kiuchumi ambayo umoja huo unaundwa. Kwa vyama vya Ushirika kilimo na Masoko idadi inayohitajika ili chama kisajiliwe ni watu kuanzia angalau hamsini (50).
Chama cha Ushirika ni kwa manufaa ya wanaushirika. Wadau wengine wanaweza kupata manufaa kutokana na shughuli za ushirika , kama vile kupata bidhaa ambazo zinatokana na shughuli za chama.
SHUGHULI:
Chama cha Ushirika cha Kilimo na Masoko dhumuni / lengo lake kuu ni kutoa huduma ya pembejeo za kilimo, kununua,kutafuta Masoko , kusindika, kusambaza na kuuza mazao ya kilimo.
UENDESHAJI:
Vyama vya Ushirika huendeshwa kwa mujibu wa masharti ya chama chenyewe, kanuni za mwaka 2004 na sheria Na. 20 ya mwaka 2003 ya vyama vya Ushirika. Ushirika huendeshwa na wanachama ambao wameuunda. Wanachama wa chama cha Ushirika ni watu wenye umri usiopungua miaka 18 wenye akili timamu wanaojishughulisha na shughuli zinazowaunganisha.
HATUA ZAKE:
Kuwe na watu ambao wako tayari kuanzisha Ushirika wa aina yoyote ile. Kwa hiari yao mfano:
Ushirika wa Kilimo na Masoko – AMCOS = wanachama 50
Ushirika wa Akiba na Mikopo (SACCOS) = wanachama 20
Ushirika wa taaluma mfano: Seremala, Ufundi washi, Umeme, Ufundi magari n.k. wanachama 20
Bustani n.k. wanachama 10.
Kuwepo kwa mkutano mkuu wa Uhamasishaji wa Ushirika
Afisa Ushirika Mtoa Elimu ya Ushirika Viongozi na wadau wengine Wahamasishaji.
Kuwepo kwa mkutano mkuu wa uanzilishi wa Ushirika:
Afisa Ushirika atakuwa mwenyekiti wa muda
Watachaguliwa viongozi wa muda (Formalization Committee)
Watapendekeza viwango vya kuchangia ilikuwa Mwanachama ikiwa ni pamoja na;
. Kiingilio - kitakachopendekezwa
. Hisa 5 @ Tshs.
. Akiba ya mwezi/mwaka Tshs.
Mapendekezo ya kuandaa Katiba/Masharti ya chama
Kuwepo kwa eneo la ofisi ya chama
Pendekezo la kufungua akaunti Benki na kuteua watia saini
Uongozi wa muda kusaidiana na Afisa Ushirika kwenye
Copyright ©2021 Wanging'ombedc . All rights reserved.