HALMASHAURI YA WILAYA YA WANGING’OMBE
IDARA YA ARDHI NA MALIASILI
VIJUE VIVUTIO VYA UTALII KATIKA WILAYA YA WANGING’OMBE
Wilaya ya Wanging’ombe imebahatika kuwa na vivutio vingi vya utalii ambavyo vinaweza kuchangia
mapato makubwa kutokana na wageni mbalimbali wanaoweza kutembelea vituo kwa ajili ya kujionea
maajabu mbalimbali katika vivutio hivyo. Vivutio vinavyopatikana katika wilaya ya Njombe ni pamoja
na Mapango na Msitu wa hifadhi wa Nyumbanitu, mwamba wenye ramani ya bara la Afrika, pori la
akiba la Mpanga Kipengere, Eneo la ardhi oevu la Lihogosa, Kilele cha mlima wa Fulanyingi, eneo la
kihistoria la Mdandu, Mapango na Msitu wa Mayiviyivi na Kanisa la kilutheri la Kidugala.
A. MAPANGO NA MSITU WA NYUMBANITU
Mapango na Msitu wa Nyumbanitu viko katika kijiji cha Mlevela, kata ya Igima tarafa ya Mdandu.
Msitu huu ni wa maajabu sana kwani miti yake na mimea yake iko pale kwa karne nyingi.
Inaaminika kuwa makabila mengi ya mikoa ya Iringa, Mbeya, Morogoro na Ruvuma yana
asili ya eneo la Nyumbanitu na kuwa wahenga wa wabena walizikwa katika eneo hili.
Sifa za Pekee za Msitu na Mapango
a. Uwepo wa eneo la Tambiko.
b. Kuwepo kwa kuku weusi ndani ya msitu wasiofugwa.
c. mapango makubwa ambayo watu zaidi ya mia moja
wanaweza kuishi kwenye mapango. Mapango hayo
yalikuwa yanatumika sana wakati wa vita.
d. Aina (Sp) pekee za miti.
Aina ya Utalii unaofaa
a. Utalii wa kiutamaduni.
b. Utalii wa kupiga picha.
c. Utalii wa kutembelea na
kupumzika kwenye mapango.
Msitu wa Nyumbanitu Msitu wa Nyumbanitu Mapango ya Nyumbanitu
S. L. P 624
NJOMBE
2
B. MWAMBA WENYE RAMANI YA BARA LA AFRIKA
Mwamba wenye ramani ya bara la Afrika uko katika kijiji cha Igodivaha, kata ya Kidugala, tarafa ya
Imalinyi. Eneo hili lina uzuri wa kipekee kimandhari na pia utashangazwa na mwamba wenye ukubwa
unaokadiriwa kuwa ekari 14 na sehemu ya mwamba huu ina sura mithili ya ramani ya bara la Afrika.
Mwamba/jiwe hili limezungukwa na msitu wa hifadhi wa Lwivala wenye miti aina ya miombo
inayofanya eneo hili kuwa tulivu na lenye mandhari nzuri.
C. PORI LA AKIBA LA WANYAMAPORI LA MPANGA/KIPENGERE
Pori hili linapatikana katika wilaya za Wanging’ombe, Makete na Mbarali. Pori hili linasimamiwa na
shirika la taifa la hifadhi ya wanyama pori (TANAPA). Pori hili lina sifa ya kuwa na mimea na
wanyama wa aina mbalimbali (baadhi wakiwa adimu). Inaaminika kuwa kuna zaidi ya aina 28 za
wanyama pori; baadhi ya wanyama hao ni nguruwe pori, ngiri, nyani, fisi, mbega wekundu,
kakakuona, na mbweha wenye mgongo mweusi. Pia wapo mamba, nyoka na ndege wa aina
mbalimbali. Katika pori hili pia kuna mandhari nzuri ya hali ya miinuko na mabonde na maporomoko
na vyanzo vya maji.
Aina ya utalii inayofaa kufanywa eneo hili ni kupiga picha, kupanda milima n.k.
Mwamba wenye ramani ya barara la Afrika
Sifa kwa shughuli za Utalii
a. Mwamba wenye ramani ya Asili.
b. Sehemu ya kufanyia Tafrija.
Aina ya Utalii Unaofaa
a. Utalii wa mazingira.
b. Utalii wa picha pamoja na
c. sehemu za kupumuzika.
Baadhi ya Maeneo ya pori la Mpanga Kipengere
3
D. ENEO OEVU LA LIHOGOSA
Eneo hili oevu la Lihogosa liko kando kando ya barabara kuu inayotoka Njombe kuelekea Makambako
na liko katika vijiji vya Igima na Mhaji.
Eneo oevu la Lihogosa limebainika kutembelewa na ndege maji wa aina mbalimbali, lina samaki, na
lina uzuri wa kipekee wa mandhari na maeneo mazuri ya tafrija. Bonde la Lihogosa lina nyasi fupi za
kijani na maji yaliyotuama.
Eneo oevu la Lihogosa linafaa kwa utalii wa uvuvi, utalii wa kuzunguka bwawa kwa kutumia
mitumbwi, kuogelea, kuona ndege, utalii wa picha na tafrija/mapumziko. Eneo hili linafaa pia kwa
uwekezaji wa lodge na campsite.
E. MLIMA FULANYINGI
Kilele cha mlima Fulanyingi kinapatikana katika kijiji cha Imalilo kata ya Wangama. Eneo hili ndio
uwanda wa juu kabisa kuliko maeneo yote ya wilaya ya Wanging’ombe na Njombe, hivyo kilele hiki
hutoa fursa ya kuona mandhari pana ya wilaya ya Wanging’ombe na maeneo mengine jirani. Pia
katika mlima Fulanyingi kuna vyanzo vingi vya maji zaidi ya 98.
Eneo hili linafaa sana kwa utalii wa kupanda milima, Kujionea wanyama na mandhari nzuri ya
maumbile ya kijiografia, sehemu za mapumziko na utalii wa picha.
Eneo la kilele hiki linafaa kwa uwekezaji wa miundombinu ya kupumzikia (campsite).
F. MAENEO YA KIHISTORIA YA MDANDU
Maeneo ya kihistoria ya Mdandu yako katika kijiji na kata ya Mdandu, tarafa ya Imalinyi. Maeneo ya
kihistoria ya Mdandu yanajumuisha Mahakama na Boma la Wajerumani, njia ya watumwa wa kabila
la Wabena, Wakinga na Wapangwa pamoja na mti aina ya Mdzombe ambao ni asili ya jina la Mkoa wa
Njombe kwa sasa.
Eneo la Mdandu lina umuhimu mkubwa kwa historia ya Mkoa wa Njombe. Hii inatokana na eneo hilo
kuwa na sifa zifuatazo:-
a. Makazi na ofisi za kwanza za utawala wa Kijerumani (German Boma). Wajerumani walichagua
Mdandu kuwa makao makuu ya wilaya ya Njombe (Mkoa wa Njombe kwa sasa). Baada ya
Wajerumani kupigwa na Waingereza katika vita kuu ya kwanza ya dunia, Waingereza
waliamua kuhamisha makao makuu ya Wilaya kuwa Njombe. Hivyo waliamua kuhamisha
’boma’ hiyo kuja mahali ilipo Njombe kwa sasa. Mahakama iliyokuwa ikitumiwa na
Wajerumani ipo hadi sasa ila haitumiki kutokana na ubovu wa jengo.
Eneo oevu la Lihogosa
4
b. Soko la Mdandu. Soko hilo lipo na halitumiki kwa madhumuni ya soko.
c. Barabara ya watumwa. Wakati biashara ya utumwa ikifanyika, watu wa Ubena, Ukinga na
Upangwa walikusanywa kutoka maeneo hayo kwenda pwani kwa ajili ya kuuzwa. Chifu wa
wabena aliyeitwa Mbeyela alishiriki biashara ya watumwa kwa kutoa ushirikiano kwa Waarabu
kwa kuwa alikuwa akipata silaha na vitu vingine kutoka kwa Waarabu.
d. Makazi ya Chifu wa Ubena. Makazi ya Chifu yapo katika eneo la Mdandu.
e. Mti wa Mdzombe. Katika eneo hili kuna mti ambao jina lake ndilo asili ya jina la Mkoa wa
Njombe. Hii inatokana na Wajerumani kushindwa kutamka jina hilo inavyostahili hivyo
kutohoa jina hilo na kuita Njombe.
Utalii unaofaa katika maeneo haya ya kihistoria ni ule wa kujifunza historia ya Wabena.
G. KANISA LA KILUTHERI LA KIDUGALA
Kanisa la Kilutheri la Kidugala liko katika kijiji na kata ya Kidugala, tarafa ya Imalinyi. Kanisa hili ni la
kihistoria na kivutio cha utalii kwa sababu zifuatazo:-
a. Kuwa na jengo lenye umri wa zaidi ya miaka 100. Kanisa la Kidugala lilikamilika kujengwa
mnamo mwaka 1898.
b. Kuwepo kwa nyaraka za kale zenye masimulizi kuhusu historia ya Wabena kama walivyokutwa
na Wajerumani na ushiriki wao katika vita ya Maji maji.
H. MSITU WA ASILI WA MAYIVIYIVI NA MAPANGO
Msitu na mapango ya Mayiviyivi yako katika kijiji cha Igagala, kata ya Ulembwe, tarafa ya Imalinyi.
Katika msitu huu kuna mapango yenye vyumba mbalimbali. Eneo la msitu na mpango ya Mayiviyivi
hutumika kwa shughuli za matambiko na ni eneo linalofaa kwa utalii wa kiutamaduni.
Kanisa la Kilutheri la Kidugala
5
CHANGAMOTO ZINAZOIKABILI SEKTA YA UTALII
a. Ukosefu wa kwa ajili ya kutekeleza shughuli za sekta ya Utalii katika wilaya, hivyo sekta hii
inategemea fedha za makusanyo ya halmashauri.
b. Kukosekana kwa huduma ya tovoti ili kurahisisha utangazaji wa vivutio ili kuweza kupata
wageni kwa urahisi zaidi.
c. Ukosefu wa wataalamu wenye fani ya Utalii katika halmashauri ya Wanging’ombe.
d. Kukosekana kwa tafiti za kina na mara kwa mara ili kupata taarifa sahihi za vivutio.
e. Kukosekana kama hotel, maeneo ya kupumzika, huduma za vyoo nk karibu na vivutio.
FURSA ZILIZOPO KATIKA MAENEO YA VIVUTIO
a. Uwezekano wa kutengeneza sehemu za huduma za kitalii kama vile maeneo ya kupumzikia
watalii, vyoo, sehemu za chakula, malazi na zile za kutupia taka.
b. Uwezekano wa kuvitangaza vivutio kitaifa na kimataifa ili kuvutia watalii wengi zaidi
kulitembelea.
MIKAKATI YA UBORESHAJI VIVUTIO VYA UTALII
a. Kushirikisha wanajamii wanaoishi katika maeneo ya vijiji vinakopatikana vivutio tajwa
kutengeneza miundombinu ya vyoo, sehemu za kupumzikia watalii, kutupia taka, kwa
kutumia raslimali zinazopatikana katika maeneo ya vijiji vyao.
b. Kuzijengea uwezo kamati za Maliasili za vijiji juu ya umuhimu wa utunzaji wa Mazingira
ya vivutio vya utalii na utunzaji wa kumbukumbu mbalimbali za utalii.
c. Kuyabainisha maeneo mbalimbali ya uwekezaji wa miundombinu ya utalii zikiwemo
hoteli za kitalii na kuwakaribisha wadau kuwekeza katika maeneo jirani na vivutio
ikiwemo maeneo ya Igodivaha – (Kata ya Imalinyi), Mlevela/Nyumbanitu- (Kata ya
Mdandu).
d. Kuandaa utaratibu wa kuvitangaza vivutio vyote vilivyopo ndani ya wilaya.
e. Kuanza mchakato wa kuandika andiko la Mapendekezo (Proposal) ya uboreshaji wa
miundombinu ya vivutio vya utalii itakayosambazwa kwa wadau mbalimbali ili
kuhamasisha uwekezaji na Uchangiaji wa uboreshaji wa miundombinu itakayobainishwa.
--------------------------
Kasmiri David
Forest Officer I - H/W
WANGING’OMBE
Copyright ©2021 Wanging'ombedc . All rights reserved.