Kitengo cha Tekinolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) ni kitengo huru chenye Mamlaka kamili katika Halmashauri ya Wilaya ya Wanging'ombe. Jukumu lake kubwa ni Kutoa Ushauri Kwa Mkurugenzi Mtendaji (W) kuhusiana na Masuala yote yanayohusiana na Mifumo ya Taarifa na Utendaji kazi.Mifumo hiyo ni mfumo wa Kuidhinisha malipo wa Epicor 9.05, mfumo wa Taarifa za Utumishi wa HCMIS/Lawson, mfumo wa Mapato LGRCIS, mfumo wa taarifa za takwimu za Idara ya Elimu wa BEMIS na PreM , Mfumo wa upangaji bajeti wa Plan Rep na mingine inayohusiana.
Sambamba na hilo, pia Kutoa Ushauri wa ujumla katika Idara na Vitengo katika Halmashauri kama vile masuala ya Manunuzi ya Vifaa bora vya Kitekinolojia na kuhakikisha matumizi sahihi na salama ya vifaa hivyo.
Malengo ya Kitengo cha TEHAMA ni kuwa na Matumizi sahihi na salama ya Tekinolojia kwa maendeleo ya Halmashauri.
Moja ya shughuli mahsusi zinazofanyika ni;
1. Kusimamia ufanisi wa mifumo yote katika Halmashauri.
2. Kutoa ushauri wa kitaalam katika Idara na vitengo.
3. Kusimamia na kuratibu mafunzo kazini juu ya masuala ya TEHAMA
Copyright ©2021 Wanging'ombedc . All rights reserved.