Idara ya Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji inashughulikia upangaji na uratibu wa mipango ya maendeleo katika miaka husika, usimamizi na ufuatiliaji wa miradi ya maendeleo ya Halmashauri, Tafiti na ukusanyaji wa Takwimu pamoja na kuratibu shughuli za Uwekezaji. Idara hii inaongozwa na Mchumi wa Halmashauri na imegawanyika katika sehemu tano kama ifuatavyo:-
Mipango na Sera
Usimamizi na Ufuatiliaji wa Miradi ya Maendeleo
Uwekezaji
Tafiti na Takwimu.
Sehemu ya TASAF
Sehemu ya Mipango na Sera.
Majukumu ya sehemu hii ni kama ifuatavyo:-
Kusimamia Uandaaji wa mpango wa utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi kila mwaka.
Kuratibu ufanisi wa mifuko ya Halmashauri: LGCDG, Mfuko wa Jimbo na fedha za mapato ya ndani.
Uratibu na utayarishaji wa Mipango shirikishi katika Kata zote za Halmashauri kupitia Mfumo wa O&OD.
Uratibu na utayarishaji wa Mpango na Bajeti ya kila mwaka ya Halmashauri.
Kusimamia uandaaji wa mipango kazi (Action Plans) ya bajeti za kila mwaka na kuziwasilisha katika ngazi husika..
Kuratibu uandaaji wa maandiko ya miradi mbalimbali ya maendeleo.
Kuratibu maandalizi na utekelezaji wa Mpango wa Matokeo Makubwa sasa (BRN)
Kuratibu maandalizi ya Sera na Mpango Mkakati wa Halmashauri
Kuratibu uandaaji wa taarifa mbalimbali za Halmashauri pamoja na taarifa za utekelezaji wa maagizo kutoka mamlaka za juu za serikali
Sehemu ya Usimamizi, Ufuatiliaji na Tathmini ya miradi ya
maendeleo.
Majukumu ya sehemu hii yapo kama ifuatavyo:-
Kuratibu uandaaji wa taarifa za Ilani ya Uchaguzi wa CCM ya 2015 - 2020
Kufuatilia utekelezaji halisi na matumizi ya fedha za miradi ya maendeleo.
Kuratibu miradi ya jumuiya za wananchi na taasisi nyinginezo za ndani na nje ikiwemo miradi ya wahisani
Kuratibu utekelezaji wa Mipango ya muda mrefu, kati na mfupi ikiwepo Ilani ya Uchaguzi na uandaaji wa taarifa za utekelezaji wa mipango hiyo
Kuratibu utekelezaji wa mipango shirikishi.
Kuandaa taarifa za Miradi ya maendeleo ya Manispaa kwa vipindi mbalimbali na kuziwasilisha kwenye mamlaka husika.
Kuandaa mapitio ya bajeti ya kila mwaka baada ya kipindi cha nusu mwaka
Kuandaa mapendekezo ya kubadili matumizi ya vifungu vya bajeti ya maendeleo kila inapobidi.
Kuandaa taarifa za matukio ya kila wiki na kuiwasilisha ngazi ya mkoa.
Sehemu ya Uwekezaji.
Sehemu hii hushughulikia mipango ya uwekezaji katika Halmashauri ya Manispaa kwa kufanya yafuatayo:-
1. Kuratibu na kusimamia maandalizi ya mipango ya uwekezaji ya Halmashauri.
2. Kuratibu utekelezaji na uandaaji wa taarifa za mipango ya uwekezaji
3. Kuratibu utekelezaji wa miradi ya DMDP
Sehemu ya Utafiti na Takwimu.
Sehemu hii hushughulikia masuala yanayohusu takwimu mbalimbali za kiuchumi na kijamii pamoja na kuratibu shughuli za utafiti kama ifuatavyo:-
Ø Kuratibu na kusimamia benki ya Takwimu ya Halmashauri ikihusisha takwimu za LGMD.
Ø Kuhuisha na kuboresha Takwimu za Kiuchumi na Kijamii (Profile) za Halmashauri.
Ø Kuratibu na kuhifadhi takwimu za Idadi ya watu za Halmashauri kwa
Ø kutumia rejista za wakazi wa Mitaa.
Ø Kuratibu na kutathmini utekelezaji wa Mpango mkakati wa Halmashauri 2012/13 – 2016/17
Ø Kuratibu zoezi la Sensa ya Watu na Makazi.
Ø Kuandaa taarifa za utatuzi wa kero na malalamiko kila wiki na kuziwasilisha kwa Mkuu wa Mkoa
Sehemu ya TASAF
Utekelezaji wa shughuli za awamu ya tatu ya TASAF Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini (TASAF III PSSN) katika Halmashauri ya Wilaya ya Wanging'ombe
Copyright ©2021 Wanging'ombedc . All rights reserved.