MKUTANO WA UZINDUZI WA KAMPENI YA KUHAMASISHA LISHE NA MPANGO WA KUONGEZA KASI YA KUPUNGUZA UDUMAVU
21 January 2024
Halmashauri ya Wilaya ya Wanging'ombe inawajulisha na kuwakaribisha wananchi wote wa Wilaya ya Wanging'ombe kuhudhuria Mkutano mkubwa wa hadhara kwa ajili ya Uzinduzi wa Kampeni ya kuhamasisha LISHE BORA KWA WATOTO na Mpango wa Kupunguza UDUMAVU.
Mkutano utafanyika Halmashauri ya Wilaya ya Wanging'ombe, siku ya Alhamisi, 25 Januari 2024 kuanzia Saa 03:00 Asubuhi.