SHUGHULI ZINAZOFANYWA NA IDARA YA MAENDELEO YA JAMII
Idara ya Maendeleo ya Jamii ni miongoni mwa Idara inayotoa huduma ya ugani katika jamii kwa kutumia njia shirikishi katika kubuni,kupanga,kutekeleza na kufuatilia miradi ya maendeleo ya jamii husika katika Wilaya ya Wanging’ombe.
Kadhalika idara inajihusisha na uhamasishaji wananchi juu ya:
i.Umuhimu wa kuchangia nguvu kazi na fedha ya miradi ya kujitegemea
ii. Kuwezesha usajili wa vikundi vya kijamii
iii. Kuwezesha kutoa mikopo yenye masharti nafuu kwa kwa vikundi vya vijana na wanawake.
iv. Kuwezesha tafiti za kijamii
v. Kuhamasisha jamii juu ya usawa wa kijinsia na kuondokana na mila na desturi zinazokwamisha maendeleo
vi. Kuelimisha jamii juu ya kuziua ukatili wa kijinsia,ukeketaji wasichana na wanawake,Ukweli kuhusu UKIMWI na kuondokana na dhana potofu za ushirikina na uchawi.
vii. Kusimamia Miradi ya ikiwemo Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF III) na wa Mapambano dhidi ya UKIMWI.
viii.Kuwezesha uhamasishaji na usajili wa Jumuiya za Watumia maji
1.0 KUSIMAMIA MIFUKO YA MAENDELEO YA WANAWAKE NA VIJANA.
Idara ya maendeleo ya Jamii inawezesha vikundi vya wanawake na vijana kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Wanawake (WDF) na Mfuko wa Maendeleo ya Vijana (YDF).
1.1 MFUKO WA MAENDELEO YA WANAWAKE
Mfuko wa Maendeleo ya Wanawake ulianzishwa Mwaka 1993 kwa azimio la Bunge “Exechequer and Audit Ordinance ya Mwaka 1961.
Mfuko huu unachangiwa 5% ya mapato ya Halmashauri na Serikali Kuu yaani Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii.
1.1.1 Lengo la Mfuko:
Walengwa wa mfuko huu ni wanawake wote wa Tanzania wenye Umri wa miaka 15 na kuendelea wenye uwezo wa kufanya kazi za uzalishaji mali.
1.1.2 SIFA ZA VIKUNDI VYA WANAWAKE
i.Kikundi cha wanawake watano(5)
ii.Kikundi kiwe kimesajiliwa na Idara ya Maendeleo ya Jamii(Halmashauri ya Wilaya/Mji)
iii. Kikundi kiwe na mradi wa kiuchumi
iii.Kikundi kimewasilisha maombi ya mkopo kupitia kwa Afisa Mtendaji wa Kijiji na Kata
iv.Kikundi kijadiliwe na kupitishwa na Kata (Kamati ya mikopo ya ngazi Kata).
v. Kamati ya mikopo ngazi ya Halmashauri itapitia na kuidhinishwa.
1.2.1 Uwezeshaji mikopo kwa Vikundi vya wanawake kiuchumi:
|
|
|
|||
|
|
|
|
||
2013/14 |
38,624,363 |
4,500,000 |
9 |
0 |
0 |
2014/15 |
40,146,300 |
10,000,000 |
12 |
0 |
0 |
2015/16 |
40,822,340 |
23,000,000 |
21 |
7,000,000 |
6 |
2016/17 |
40,500,000 |
44,500,000 |
35 |
0 |
0 |
JUMLA |
160,093,003
|
82,000,000
|
77
|
7,000,000 |
6 |
Katika kipindi cha Mwaka 2013/14 hadi 2017 jumla ya vikundi 83 vya Wanawake vimewezeshwa Jumla ya Tsh 82,000,000 kutokana na mchango wa mapato ya ndani Halmashauri na toka Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto.
1.2.0 Mfuko wa Maendeleo ya Vijana
1.2.1 Mfuko wa Maendeleo ya Vijana ulianzishwa Mwaka 1993/94 chini ya kifungu cha Na.17(i) cha The Exchequer and Audit ordinance (cap.439) Na,21 of 1961”
1.2.2 Walengwa wa mfuko huu ni:
Mwaka |
Bajeti |
Kiasi cha Mikopo |
|||
Halmashauri |
vikundi |
Serikali Kuu |
Vikundi |
||
2013/14 |
38,624,363 |
4,500,000 |
6 |
0 |
0 |
2014/15 |
40,146,300 |
10,000,000 |
18 |
0 |
0 |
2015/16 |
40,822,340 |
21,000,000 |
7 |
0 |
0 |
2016/17 |
40,500,000 |
29,500,000 |
22 |
0 |
0 |
JUMLA |
160,093,003
|
65,000,000
|
53
|
0 |
0 |
1.2.3 Sifa ya Wakopaji:
Katika kipindi cha Mwaka 2013/14 hadi 2017 jumla ya vikundi 53 vya Vijana vimewezeshwa Jumla ya Tsh 61,000,000 kutokana na mchango wa mapato ya ndani Halmashauri.
Kikundi vya wanachama watano,na wawe na shughuli wanazozifanya za kujiiongezea kipato
2.2 SIFA ZA WAKOPAJI
Mkopaji (Vikundi) wanapaswa kurudisha kiasi cha fedha kinachotakiwa kurejeshwa kwa robo husika katika SACCOs aliyopokelea mikopo.
Mikopo hii hutozwa riba ya 10% inayolipwa Halmashauri na 2% kwa vyama vya ushirika vya kuweka na kukopa(SACCOS) na kufanya riba ya 12% katika muda ndani ya miezi 12 (mwaka mmoja) ambayo imegawanyika kwa robo 4 kila robo.
Fedha za Mikopo hii hutokana na mchango wa Halmashauri tokana 5% ya mapato yake ya ndani.
Mikopo ya Mfuko wa Maendeleo ya Wanawake hutolewa kupitia vyama vya ushirika (SACCOS) vilivyo karibu na Kijiji kinapotoka kikundi husika, hii inasaidia ufuatiliaji wa vikundi na marejesho ya mikopo kwa kuwa fedha hizi ni mfuko maalum (revolving Fund) ni lazima waliokopeshwa warudishe ili vikundi vingine vikopeshwe.
2.1. UTARATIBU WA UTOAJI MIKOPO(WDF)
2.0 MFUKO WA MAENDELEO YA WANAWAKE(WDF)
Uwezeshaji mafunzo ya ujasiriamali kwa Vikundi vya Vijana katika Kijiji cha Katenge Kata ya Wanging’ombe.
Na.
|
JINA LA MRADI
|
WALENGWA
|
KIJIJI
|
KATA
|
|
1
|
Ufugaji wa Mbuzi
|
i.
|
Vikundi 4
|
Igando
|
Luduga
|
|
|
ii.
|
Vikundi 2
|
Sakalenga
|
Itulahumba
|
|
|
iii.
|
Vikundi 3
|
Mpululu
|
Udonja
|
2.
|
Ujenzi wa nyumba
|
iv
|
Mwalimu S/M
|
Ivigo
|
Igosi
|
3.
|
Ujenzi wa madarasa S/M
|
v.
|
Wanafunzi S/M
|
Msimbazi
|
Uhambule
|
Katika kipindi cha Mwezi Septemba,2017 Halmashauri imepokea fedha kwa ajili ya Miradi mikuu 3 ya ufugaji mbuzi,ujenzi wa nyumba ya Mwalimu Shule ya Msingi Ivigo na Ujenzi wa madarasa ya Shule ya Msingi Msimbazi ambayo imetambulishwa na kuingiziwa fedha kiasi cha Jumla Tsh.235,079,737.57 kwa ajili ya utekelezaji kama ifuatavyo:
3.3. UTAMBUZI WA MIRADI
MPANGO WA TASAF III: Kikundi cha (kuweka na kukopa) COMSIP Kijiji cha Mayale:Agosti,2017
TASAF III (OPEC): Mradi wa ufugaji Kuku Bi. Asia Ngole Kijiji cha Mayale: Agosti,2017
Mpango wa TASAF III: Nyumba ya Walimu Shule ya Sekondari Usuka-Kata ya Usuka: Agosti,2017
Mpango wa TASAF: Wanakikundi wakikamilisha ujenzi wa kivusha maji cha Mfereji wa umwagiliaji Kijiji cha Mtapa: Agosti,2017
Bi.Anna Mwinuka mlengwa wa TASAF III(OPEC) anafanya biashara ya mayai ya kuku wa kienyeji na anajenga nyumba ya kisasa Kijiji cha Mayale: Septemba,2017.
Mpango wa TASAF III(OPEC) Bi.Anna Mwinuka Kijiji cha Mayale akifanya biashara ya mayai ya kuku wa kienyeji.
No
|
KATA
|
Kijiji
|
Jina la Mradi
|
Kiasi kilichotengwa
|
Hatua za utekelezaji
|
1
|
Igwachanya
|
Mtapa
|
Kivusha maji ya mfereji wa umwagiliaji
|
66,389,360.71
|
Ujenzi umekamilika. Maandalizi ya vyeti vya kuzindua miradi inaendelea.
|
2
|
Mdandu
|
Itambo
|
Ufugaji wa mbuzi na Kuku
|
22,321,428.56
|
Mradi umekamilika. Maandalizi ya vyeti vya kuzindua miradi inaendelea.
|
3
|
Kidugala
|
Masage
|
Ufugaji wa mbuzi,kuku na nyuki
|
22,321,428.56
|
Mradi umekamilika. Maandalizi ya vyeti vya kuzindua miradi inaendelea.
|
4
|
Wanging’ombe
|
Mayale
|
Ufugaji wa kuku na mbuzi
|
22,321,428.56
|
Mradi umekamilika. Maandalizi ya vyeti vya kuzindua miradi inaendelea.
|
5
|
Kijombe
|
Lyamluki
|
Ufugaji Kuku,mbuzi na nyuki
|
22,321,428.56
|
Mradi umekamilika. Maandalizi ya vyeti vya kuzindua miradi inaendelea.
|
6
|
Saja
|
Igenge
|
Nyumba ya walimu Sekondari
|
66,389,360.71
|
Ujenzi umekamilika. Maandalizi ya vyeti vya kuzindua miradi inaendelea.
|
7
|
Usuka
|
Usuka
|
Nyumba ya walimu Sekondari
|
66,389,360.71
|
Ujenzi umekamilika. Maandalizi ya vyeti vya kuzindua miradi inaendelea.
|
Kadhalika kupitia mpango wa TASAF III, miradi mbalimbali ya kukuza kipato,uboreshaji miundombinu ya elimu na afya na ajira za muda(walengwa) imeendelea kutekelezwa ikifadhiliwa na OPEC III.
3.2 MIRADI YA KUONGEZA KIPATO CHA KAYA MASIKINI
MUDA |
WALENGWA WALIOKUSUDIWA |
WALENGWA WALIOLIPWA |
KIASI KILICHOLIPWA |
07/08/2015
|
4,998 |
4,924 |
158,584,000 |
09/10/2015
|
4,988 |
4,971 |
145,976,000 |
11/12/2015
|
4,973 |
4,967 |
145,788,000 |
01/02/2016
|
4,998 |
4,947 |
145,456,000 |
03/04/2016
|
4,937 |
4,920 |
142,988,000 |
05/06/2016
|
4,937 |
4,920 |
142,988,000 |
07/08/2016
|
4,937 |
4,893 |
142,444,000 |
09/10/2016
|
4,907 |
4,876 |
141,900,000 |
11/12/2016
|
4,880 |
4,872 |
142,632,000 |
01/02/2017
|
4,926 |
4,881 |
133,414,000 |
03/04/2017
|
4,878 |
4,843 |
131,028,000 |
05/06/2017
|
4,827 |
4,797 |
132,412,000 |
07/08/2017
|
4,894 |
4,784 |
134,782,000 |
JUMLA KUU |
1,840,392,000 |
Hali ya utoaji fedha za Mpango wa kunusuru kaya Masikini Wilayani Wanging’ombe ni kama ifuatavyo:
Katika Wilaya ya Wanging’ombe mpango huu ulianza Mwaka 2015 kwa kufanya utambuzi na uandikishaji wa Kaya maskini ambapo malipo ya kwanza kwa kaya stahiki yalianza rasmi Mwezi Julai,2015.
Mpango huu ulizinduliwa Kitaifa katika Manispaa ya Dodoma na Mhe.Raisi Mstaafu Dkt. J.M.Kikwete mnamo Mwezi Agosti,Mwaka 2012.
3.1 Mpango wa kunusuru kaya masikini unalenga kuhawilisha fedha kwa Kaya maskini ili kujikwamua kiuchumi na kuimarisha elimu na afya bora kwa watoto ikilenga kuboresha miundombinu ya elimu,maji na afya.
3.0 MPANGO WA KUNUSURU KAYA MASKINI (TASAF III)
Mikopo hii hurudishwa ndani ya muda wa miezi 12 (mwaka mmoja) ambayo imegawanyika kwa robo 4 kila robo mkopaji anapaswa kurudisha kiasi cha fedha kinachotakiwa kurudishwa kwa robo husika.
Mikopo hii hutozwa riba ya 10% ambazo hurudishwa Halmashauri kwa ajili ya ufuatilijai mikopo na 2% hutozwa kwa ajili ya kuviwezesha vyama vya ushirika(SACCOs) na kufanya 12%.
Mikopo inayotolewa na Halmashauri ni lazima ipitie kwenye vyama vya ushirika (SACCOS) vilivyo karibu na kijiji kinapotoka kikundi husika, hii huwezesha urahisi wa ufuatiliaji wa vikundi na urejeshaji wa mikopo kwani mikopo hii ni`revolving Fund’ ni lazima waliokopeshwa warudishe ili vikundi vingine vinufaike na mikopo hii.
2.3 UTARATIBU WA UREJESHAJI
Watalaam wa Idara ya Maendeleo ya Jamii wakitoa mafunzo ya ujasiriamali kwa Wanavikundi vya Wanawake cha Amani Women Group na Tuinuane Ujindile- Kata ya Uhambule Januari,2017
Uhamasishaji Vikundi vya Wanawake na maonyesho ya shughuli za uzalishaji mali za Vikundi siku ya Wanawake Duniani 8 Machi,2017 Kijiji cha Igwachanya.
Hali ya utoaji wa mikopo kwa vikundi inakabiliwa na uchache wa fedha hivyo mikopo inayolewa ni kidogo na kwa vikundi vichache kwa sababu Halmashauri inakabiliwa na majukumu ya lazima ya uendeshaji kutokana na mapato ya ndani kutumika kwa gharama za uendeshaji wa Halmashauri ambayo pia ni mpya na maelekezo ya lazima ikiwemo upelekaji 60% ya mapato ya ndani ya Halamashauri kwa ajili ya shughuli za Maendeleo ngazi ya jamii.
Vikundi cha Wanawake TUINUANE-Uhambule na Amani Group–Ujindile Kata ya Uhambule wakipatiwa mafunzo ya uongozi,ujasiriamali na taratibu za mikopo Januari, 2016.
Copyright ©2021 Wanging'ombedc . All rights reserved.