TANGAZO KUHUSU VIWANJA VYA UFWALA - WANGING'OMBE 2025.
Tarehe iliyowekwa: September 11th, 2025
OFISI ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Wanging'ombe inawatangazia watu wote waliopewa viwanja vya Ufwala - Wanging'ombe, kwa mujibu wa mkataba walitakiwa kulipa ndani ya siku 90 kuanzia tarehe 06 Juni 2025 hadi 06 Septemba 2025. Siku zimeisha na viwanja hivyo watapewa watu wengine.
Watu wenye nia ya kufanya maombi mapya ya viwanja hivyo, mnakaribishwa.
Fika Ofisi ya Mkurgenzi Mtendaji, Halmashauri - Idara ya Ardhi ujipatie fomu ya maombi kwa ada ya Tshs. 20,000/=. Karibuni nyote.