KAMATI YA USALAMA WILAYA YARIDHISHWA NA MIRADI SEKTA YA AFYA NA ELIMU - WANGING'OMBE.
Tarehe iliyowekwa: October 6th, 2025
Na. Nickson Kombe,
KAMATI ya Ulinzi na Usalama wilaya ya Wanging’ombe imetembelea miradi 5 yenye jumla ya thamani Bilioni 2.6 ambapo vituo vya afya 3, shule za msingi 2 na kuridhishwa na hatua za ujenzi zilizofikiwa kwa sasa ikiwa pamoja na kuhamasisha uharaka wa utekelezaji wa miradi hiyo ili ianze kuhudumia jamii.
Ikiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Wanging’ombe, Mhe. Zakaria Mwansasu ametoa wito ya kuwa asiwepo mkandarasi au mzabuni ambaye atachelewesha hatua za miradi hiyo ikiwa pamoja na kuongeza idadi ya mafundi haswa hatua za kumalizia miradi hiyo ili kufikia lengo la miradi yenye ubora na kuendana na thamani ya fedha zilizotolewa.
Wito huo umetolewa na Mhe. Mwansasu, Mkuu wa Wilaya ya Wanging’ombe wakati Kamati ya Ulinzi na Usalama wilaya wakifanya ziara ya ukaguzi wa Miradi ya ujenzi wa vituo vya afya vya kata za Igosi, Luduga na Uhambule, shule za msingi mkondo B kata za Imalinyi na Igosi ambapo wajumbe wa kamati hiyo wameonyesha kuridhishwa kwa hatua za ujenzi zilizofikiwa.
Ikumbukwe miradi hii inatekelezwa na Force account na kwa sasa kituo cha afya kata ya Igosi kimefikia asilimia 74.6, kituo cha afya Uhambule kimefikia takribani asilimia 70.5, Kituo cha afya Luduga kimefikia asilimia 62.4, shule ya msingi imalinyi mkondo B imefikia asilimia 39.2 na shule ya msingi igosi mkondo B imefikia asilimia 22.4.
Aidha Idara za Afya na Elimu Msingi zimeaswa kuendelea kushirikiana kikamilifu na kitengo cha huduma za sheria halmashauri ili kuhuisha mikataba ya wakandarasi na zoezi la ukamilishaji litekelezwe Kadiri kalenda ya miradi hiyo inavyohitaji, lengo ikiwa ni kutoa huduma kwa wananchi kadiri mipango ya Serikali.