WAFANYAKAZI CRDB WANGING’OMBE WAWEZESHA WANAFUNZI WENYE UHITAJI, S/S IGIMA.
Tarehe iliyowekwa: October 8th, 2025
Na. Nickson Kombe,
KUELEKEA Kilele cha wiki ya Huduma kwa Wateja duniani, Meneja Tawi la Benki ya CRDB, Bw. Fred Mahenge akiambatana na baadhi ya wafanyakazi wameshiriki zoezi la kuwawezesha wanafunzi wenye uhitaji katika shule ya sekondari ya Igima wilayani Wanging’ombe.
Akizungumza na wanafunzi hao pamoja na uongozi wa shuleni hapo, Bw. Fred Mahenge amesema lengo ni kuongeza ufaulu mashuleni kwa kuhamasisha wanafunzi kuendelea kupenda masomo pia kuwasaidia ili kufikia ndoto zao. Hivyo ameomba wanafunzi hao waliowezeshwa kila mwanafunzi pair/jozi mbili za Sare za Shule (Uniforms), viatu, masweta, sabuni n.k kuweka juhudi kwenye masomo yao, kwani Fahari ya wafanyakazi wa CRDB ni kuona wanafunzi hao wanafaulu na kusonga mbele kimasomo.
Zaidi ya wanafunzi 20 wamewezeshwa vifaa, sare za shule (uniforms), viatu, masweta, sabuni vyote vyenye jumla ya thamani ya millioni 2.5 kiasi ambacho wamejitolea wafanyakazi wa benki ya CRDB wilaya ya Wanging’ombe.
Aidha Maadhimisho ya wiki ya Huduma kwa wateja duniani yenye kauli mbiu: “Mission Possible” ikiwa na maana “Dhamira inayowezekana” na kwa upande benki ya CRDB wanasema mafanikio ya Benki yao katika kipindi cha miaka 30 yametokana na kuzingatia maoni ya wateja pia wamejifunza kuwa kila changamoto ni fursa ya kuboresha zaidi huduma zao na kuthibitisha kwamba Mission Possible si maneno tu, bali ni utamaduni wa Benki yao.