KATIBU Tawala, Wilaya ya Wanging'ombe, Bi. Veronica Gerald Sanga anaungana na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwatakia Heri ya Mwaka mpya 2026 wananchi wa wilaya ya Wanging'ombe na watanzania wote kwa ujumla.
Watumishi wote kutoka Serikali Kuu, Serikali za Mitaa, Vyombo vya Ulinzi na Usalama na Taasisi za Umma wapo pamoja nanyi, kusikiliza sauti zenu, tunaelewa mahitaji yenu na tunachukua hatua mahususi ili kusimamia usalama na ulinzi, kukuza uchumi na shughuli za maendeleo, maboresho sekta ya elimu na kuboresha afya za wananchi wetu.
Tuendelee kulinda amani, kuimarisha umoja na kujenga kwa vitendo mustakabali wa matumaini ya Taifa letu.
Copyright ©2021 Wanging'ombedc . All rights reserved.