SALAMU ZA MWAKA MPYA 2026: MKUU WA WILAYA YA WANGING'OMBE.
Tarehe iliyowekwa: January 1st, 2026
HESHIMIWA Zakaria Saili Mwansasu anaungana na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwatakia Heri ya Mwaka mpya 2026 wananchi wa wilaya ya Wanging'ombe na watanzania wote kwa ujumla.
Wilaya ya Wanging'ombe iko pamoja nanyi, kusikiliza sauti zenu, tunaelewa mahitaji yenu na tunachukua hatua mahususi ili kusimamia usalama na ulinzi, kukuza uchumi na shughuli za maendeleo, maboresho sekta ya elimu na kuboresha afya za wananchi wetu.
Tuendelee kulinda amani, kuimarisha umoja na kujenga kwa vitendo mustakabali wa matumaini ya Taifa letu.