SALAMU ZA MWAKA MPYA 2026: MKURUGENZI MTENDAJI, HALMASHAURI YA WILAYA YA WANGING'OMBE.
Tarehe iliyowekwa: December 31st, 2025
Mimi Dkt. Peter Maiga Nyanja naungana na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwatakia Heri ya Mwaka mpya 2026 wananchi wa Wanging'ombe na watanzania wote kwa ujumla.
Halmashauri ya wilaya ya Wanging'ombe iko pamoja nanyi. Tunasikiliza sauti zenu, tunaelewa mahitaji yenu na tunachukua hatua mahususi ili kukuza uchumi, shughuli za maendeleo na kuboresha afya za wananchi wetu.
Tuendelee kulinda amani, kuimarisha umoja na kujenga kwa vitendo mustakabali wa matumaini ya Taifa letu.