SALAMU ZA MWAKA MPYA 2026: MWENYEKITI WA HALMASHAURI, WANGING'OMBE.
Tarehe iliyowekwa: January 1st, 2026
MHESHIMIWA Agnetha Mpangile anaungana na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwatakia Heri ya Mwaka mpya 2026 wananchi wa wilaya ya Wanging'ombe na watanzania wote kwa ujumla.
Mimi (Mhe. Agnetha) pamoja na madiwani wote tunaounda Baraza la Madiwani la Halmashauri ya wilaya ya Wanging'ombe tunawaahidi kuwawakilisha vyema na kuwatumikia wananchi kutoka kata zote 21 za Wilaya ya Wanging'ombe.
Tupo pamoja nanyi, kuwasikiliza sauti zenu, tunaelewa mahitaji yenu na tunachukua hatua mahususi ili kusimamia kukuza uchumi na shughuli za maendeleo, maboresho sekta ya elimu na kuboresha afya za wananchi wetu.
Tuendelee kulinda amani, kuimarisha umoja na kujenga kwa vitendo mustakabali wa matumaini ya Taifa letu.