MAKABIDHIANO YA OFISI YA MKURUGENZI MTENDAJI, WANGING'OMBE
Tarehe iliyowekwa: January 13th, 2024
Na. Mwandishi Wetu,
Nickson Kombe,
KATIBU Tawala, Mkoa wa Manyara, Bi. Maryam Muhaji (Aliekuwa Mkurugenzi Mtendaji, Wanging'ombe kabla ya Teuzi) amesaini Makabrasha ya Makabidhiano ya Ofisi ya Mkurugenzi ambapo kwa sasa amekabidhiwa Dkt. Peter Maiga Nyanja (Mkurugenzi Mtendaji, Wanging'ombe baada ya Teuzi) katika hafla fupi iliyofanyika Ukumbi wa Halmashauri.
Akiongea na Watumishi waliohudhuria hafla hiyo, Bi. Maryam Muhaji (Katibu Tawala, Manyara) ametoa neno la shukrani kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuonyesha imani na utendaji wake na kumteua kuwa Katibu Tawala ila pia Watumishi na Baraza la Madiwani Wanging'ombe kwa ushirikiano waliompatia kwa muda wake wote wa Utumishi katika Halmashauri.
Aidha Hafla fupi za Makabidhiano ya Ofisi ya Mkurugenzi zimehudhuriwa na Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri, Diwani Kata ya Imalinyi, Mhe. Onesmo Lyandala, Katibu Tawala, Wilaya ya Wanging'ombe, Bi. Veronica Sanga, Mkurugenzi Mtendaji, Wanging'ombe, Dkt. Peter Maiga Nyanja pamoja na Wakuu wa Divisheni/Vitengo na Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Wanging'ombe.