Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Wanging'ombe anapenda kuwatangazia wananchi wote wa Wilaya ya Wanging'ombe kuwa Mwenge wa Uhuru utakimbizwa katika Wilaya yetu tarehe 30/04/2017. Mwenge wa Uhuru utakabidhiwa Wilayani Wanging'ombe katika kijiji cha Igenge na kukimbizwa katika vijiji vya Idenyimembe,Saja,Uhenga,Wanging'ombe,Mayale Ilembula ambapo Mwenge huo utakesha.Mkurugenzi Mtendaji anapenda kuwaomba Wananchi wote wa Wilaya ya Wanging'ombe kujitokeza kwa wingi kuulaki Mwenge wetu wa Uhuru utakao fungua ,kagua na kuweka mawe ya Msingi katika miradi mbalimbali inayotekelezwa katika Wilaya yetu.
Copyright ©2021 Wanging'ombedc . All rights reserved.