HALMASHAURI YA WILAYA YA WANGING’OMBE
Barua zote ziandikwe kwa Mkurugenzi Mtendaji (W)
S.L.P 64,
NJOMBE
Unapojibu tafadhali taja;-
Kumb. Na. WDC/F.20/123 25.08.2017
TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI.
1. UTANGULIZI.
Halmashauri ya Wilaya Wanging’ombe ni moja kati ya Halmashauri sita zilizopo kwenye Mkoa wa Njombe. Makao Makuu yake yapo katika Kata ya Igwachanya, Kijiji cha Igwachanya. Halmashauri ya Wilaya ya Wanging’ombe inakua kwa kasi kiuchumi na hii ni kutokana na kuboreka kwa shughuli za kiuchumi, mawasiliano na muingiliano wa watu. Sehemu kubwa ya uchumi inategemea kilimo cha mazao ya biashara kama vile Mahindi, Maharage, Miti, Alizeti, Viazi n.k.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Wanging’ombe anawatangazia Wananchi wote Raia wa Tanzania wenye sifa kuomba kujaza nafasi zifuatazo.
2. MTENDAJI WA KIJIJI DARAJA LA III – TGS B (NAFASI 52).
2.1. Sifa za Muombaji;
Awe na Elimu ya Kidato cha Nne (Form IV) au Sita (Form VI) aliyehitimu mafunzo ya Astashahada/Cheti katika moja ya fani za Utawala, Sheria, Elimu ya Jamii, Usimamizi wa Fedha, Maendeleo ya Jamii na Sayansi ya Sanaa kutoka Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo, Dodoma au Chuo chochote kinachotambulika na Serikali.
2.2. MSHAHARA.
Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani Mshahara wa TGS B
2.3. KAZI NA MAJUKUMU
i. Afisa Masuuli na Mtendaji Mkuu wa Serikali za Kijiji,
ii. Kusimamia Ulinzi na Utawala Bora wa Raia na mali zao, kuwa mlinzi wa amani na msimamizi wa utawala bora katika Kijiji,
iii. Kuratibu na kusimamia upangaji wa utekelezaji wa mipango ya Maendeleo ya Kijiji,
iv. Katibu wa Mikutano na Kamati zote za Halmashauri ya Kijiji,
v. Kutafsiri na kusimamia Sera na Taratibu,
vi. Kuandaa taarifa za utekelezaji na kazi katika eneo lake na kuhamasisha uchumi katika kuandaa na kutekeleza mikakati ya kuondoa umasikini na kuongeza uzalishaji mali,
vii. Kiongozi na mkuu wa Idara na Vitengo vya Kitaalam katika Kijiji,
viii. Kusimamia, kukusanya na kuhifadhi kumbukumbu na nyaraka za kijiji,
ix. Kujibu na kuandaa taarifa za utekelezaji wa kazi katika eneo lake na kuziwasilisha kwenye Halmashauri ya Kijiji na baadaye kwenye Mkutano Mkuu wa Kijiji na Kamati ya Maendeleo ya Kata,
x. Kupokea, kusikiliza na kutatua migogoro ya wananchi,
xi. Kusimamia utungaji na utekelezaji wa Sheria ndogo za Kijiji,
xii. Kusimamia ukusanyaji wa mapato katika kijiji,
xiii. Atawajibika kwa Mtendaji wa Kata na Mkurugenzi Mtendaji.
xiv. Kuandaa na kutunza rejesta ya wakazi wote Kijiji
3.0 DEREVA DARAJA LA II – TGOS A (NAFASI 2).
3.1 Sifa za Muombaji;
i. Awe mwenye cheti cha kidato cha Nne (Form IV) na leseni ya daraja E au C1 ya uendeshaji Magari ambaye amefanya kazi kwa muda usiopungua mwaka mmoja bila kusababisha ajali.
ii. Awe amehudhuria mafunzo ya msingi ya uendeshaji magari (Basic Driving Course) yanayotolewa na Chuo cha Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) au Chuo kingine kinachotambuliwa na Serikali.
iii. Waombaji wenye cheti cha majaribio ya Ufundi Daraja la II watafikiriwa kwanza.
3.2 MSHAHARA.
Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani Mshahara wa TGOS A
3.3. Kazi na Majukumu;
i. Kukagua gari kabla na baada ya safari ili kubaini hali ya usalama wa gari,
ii. Kuwapeleka watumishi maeneo mbali mbali kwenye safari za kikazi,
iii. Kufanya matengenezo madogomadogo ya gari,
iv. Kukusanya na kusambaza nyaraka mbalimbali,
v. Kujaza na kutunza taarifa za safari zote katika daftari la safari,
vi. Kufanya usafi wa gari,
vii. Kufanya kazi zingine kadri atakavyoelekezwa na msimamizi wako.
4.0 MASHARTI YA JUMLA KWA KAZI ZOTE.
i. Waombaji wote wawe Raia wa Tanzania na wenye Umri usiozidi miaka 45,
ii. Waombaji wote waambatanishe cheti cha kuzaliwa,
iii. Waombaji waambatanishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V.) yenye anuani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (referees) watatu wa kuaminika,
iv. Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma, maelezo, nakala za vyeti vya kidato cha nne na cha sita kwa wale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika.
v. Testimonials, “provisional results”, “statement of results”, hati ya matokeo ya kidato cha nne na sita HAVITAKUBALIWA.
vi. Waombaji waambatishe picha moja ya “Passport size” ya hivi karibuni,
vii. Mwisho wa kutuma maombi ya kazi ni tarehe 08 Septemba, 2017.
Maombi yote yatumwe kwa:-
Mkurugenzi Mtendaji (W),
Halmashauri ya Wilaya Wanging’ombe,
S.L.P. 64,
NJOMBE.
Imetolewa na:
MKURUGENZI MTENDAJI
HALMASHAURI YA WILAYA WANGING’OMBE
Copyright ©2021 Wanging'ombedc . All rights reserved.