ZIARA YA UKAGUZI WA MIRADI (KFUM), MRADI WA STENDI YA MABASI, IGWACHANYA - WANGING'OMBE
Tarehe iliyowekwa: February 9th, 2024
Na. Nickson Kombe,
WAJUMBE wa Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango (KFUM) wameridhishwa na maendeleo ya Mradi wa Stendi ya Mabasi, Igwachanya kwa Awamu ya Kwanza ya utekelezaji wake.
Akiongea na Timu ya Wataalamu (CMT) wakiongozwa na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri, Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri, Diwani Kata ya Imalinyi, Mhe. Onesmo Lyandala ameshauri umuhimu wa kuweka mfumo rasmi wa mifereji ya maji katika Awamu ya Pili ili kudhibiti hali ya kujaa maji haswa kipindi cha mvua.
Hata hivyo Kaimu Mkurugenzi Mtendaji, Bw. Kenneth Mugina amesema mradi wa stendi ya mabasi unatekelezwa na fedha zitokanazo na mapato ya ndani hivyo wameangazia kuendelea na Awamu ya Pili ya Mradi ambapo utahusisha Ujenzi wa Uzio eneo lote, Mageti Mawili ya Kuingia Stendi na Kutoka, Sakafu ya Pavels eneo lote la Stendi, Mabanda ya Kisasa ya Biashara kuzunguka Stendi ya Mabasi na Uboreshaji ambao Wajumbe wa Kamati wameshauri kutekelezwa.
Awamu ya Kwanza ya Utekelezaji wa Mradi wa Stendi ya Mabasi umekamilika ambapo umekuwa na Jengo la kupumzikia Abiria na Wasafiri, Vyoo vya Kisasa vyenye matundu - 12, Ofisi za Watendaji/Wasimamizi wa Stendi hiyo, Huduma za Maji, Safi na Salama na Miundombinu ya Umeme.
Aidha Sambamba na Utekelezaji wa Awamu ya Pili ya Mradi wa Stendi ya Mabasi Igwachanya, Halmashauri inatazamia kufanya Stendi hiyo kuwa fursa kwa wajasiriamali, wafanyabiashara na kurahisisha huduma za usafirishaji wa abiria Igwachanya.