Ziara ya Balozi wa Japan, Bw. Yasushi Misawa ametembelea mradi wa Zahanati ya Itambo, Kijiji cha Itambo, Kata ya Mdandu, Wilaya ya Wanging'ombe.
Akiongea na wananchi katika hafla fupi ya kumkaribisha kijijini hapo, iliyofanyika Zahanati ya Itambo, Balozi Misawa amewahimiza wananchi wa Itambo kufanya kazi kwa juhudi ili kuleta maendeleo ya familia na nchi ya Tanzania, kwani akiangalia taswira na mandhari ya kijijini hapo haina tofauti sana na miaka 50 iliyopita huko nchini Japan.
Mradi wa Zahanati ya Itambo ni mradi uliotekelezwa mwaka 2012 kwa msaada wa mfuko wa maendeleo wa Japan, hivyo umeleta tija na kusaidia wananchi wa Kijiji cha Itambo kupata huduma za afya na matibabu mbalimbali karibu zaidi tofauti na ilivyokuwa hapo awali iliwalazimu kusafiri umbali mrefu kwa ajili ya kupata huduma za afya.
Kwa niaba ya Wananchi, Diwani Kata ya Idandu, Mhe. AnaUpendo Gombela ametoa neno la shukrani kwa ujio huo ambao utaimarisha uhusiano baina ya Ofisi ya Balozi na wananchi wa Kijiji cha Itambo.
Aidha Balozi Misawa ameambatana na Mkurugenzi Mtendaji, Wilaya ya Wanging'ombe, Bi. Maryam Muhaji, Mganga Mkuu wa Wilaya ya Wanging'ombe, Bw. Frank Chiduo, Diwani Kata ya Idandu, AnaUpendo Gombela na Mfasiri wake Bw. Chriss.