• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe za watumishi |
Wanging'ombe District Council
Wanging'ombe District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Wanging'ombe

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati ya Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Kilimo
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii
      • Idara ya Mipango na Ufuatiliaji
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara ya Ujenzi
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Mazingira
      • Idara ya Ardhi na Maliasili
      • Utawala na Rasilimali Watu
    • Kitengo
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Manunuzi na Ugavi
      • Kitengo cha Nyuki
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Uchaguzi
      • Mawasiliano Serikalini
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Huduma
    • Huduma ya Maji
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha uongozi na Mipango
      • Kamati ya UKIMWI
      • Maadili
      • Uchumi,Afya na Elimu
    • Orodha ya Madiwani
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kumwona Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Miongozo
    • Fomu za Maombi
    • Gazeti la Serikali
    • Sheria ndogo za Halmashauri
    • Mpango mkakati wa Halmashauri
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Matukio
    • Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Hotuba

Waziri Mkuu Akutana Na Rais Wa FIFA.

Tarehe iliyowekwa: February 23rd, 2018

SERIKALI ya Tanzania inalipongeza Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) kwa jitihada na hatua mbalimbali zinazochukuliwa na shirikisho hilo katika mapambano dhidi ya rushwa.


Kauli hiyo imetolewa jana (Alhamisi, Februari 22, 2018) na Waziri Mkuu  Kassim Majaliwa katika kikao chake na Rais wa FIFA Bw. Gianni Infantino kilichofanyika jijini Dae es Salaam.


“Serikali  tunaunga mkono mapambano dhidi ya rushwa kwenye michezo pamoja na matumizi mabaya ya fedha na ya madaraka yanayofanywa na FIFA”.


Waziri Mkuu amesema wanaunga mkono mapambano hayo ili Taifa liweze kupata mafanikio makubwa katika mpira wa miguu ikiwa ni pamoja na kupata viongozi wenye maono ya mbali katika kuendeleza mchezo huo.


Amesema FIFA ambayo ni kitovu cha mapambano dhidi ya rushwa kwenye michezo , hivyo Tanzania inaiunga mkono kwa kuhakikisha sekta ya michezo inatumia vizuri fedha zilizopo kwa ajili ya kuendeleza michezo.


Waziri Mkuu amesema Serikali itahakikisha inasimamia matumizi sahihi ya madaraka katika sekta ya michezo nchini ili kuleta maendeleo kwenye mpira wa miguu.


Serikali inaipongeza FIFA kwa jitihada za dhati za kuendeleza mpira wa miguu duniani kwa kuwa mipango mbalimbali ya kuendeleza mpira wa miguu kwa vijana wadogo wa kike na wa kiume nchini.


“Tunatambua msukumo wa FIFA wa kuendelea mpira wa miguu duniani ikiwa ni pamoja na kuboresha viwanja vya michezo pamoja na maendeleo yote wanayoyafanya katika sekta hiyo.


Pia ameishukuru FIFA kwa kuipa Tanzania heshima ya kuwa mwenyeji wa mashindano ya vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 yatakayofanyika mwakani jijini Dar es Salaam na kwamba Serikali itayasimamia vizuri na inajiandaa kwa kushinda.


Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amemshukuru Rais wa FIFA Bw. Infantino kwa niaba ya Rais Dkt John Magufuli kwa kuendesha mkutano mkubwa wa viongozi wa mpira wa miguu duniani Tanzania. Mkutano huo ulihusisha Marais na Makatibu Wakuu wa nchi 21.


Pia alimpongeza Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) Bw. Ahmad Ahmad kwa jitihada zake za anazozifanya katika kuendeleza mpira barani Afrika na kwamba Serikali  ya Tanzania inamuunga mkono.


Rais wa FIFA Bw. Infantino ambaye ameahidi kuisaidia Tanzania kwa kuboresha miundombinu ya viwanja vya michezo aliwasili nchini leo alfajiri akiongozana na Rais wa Shirikisho la Soka Afrika Bw. Ahmad Ahmad kwa ajili ya mkutano wa FIFA uliofanyika nchini Tanzania February 22, 2018.


Bw. Infantino amewasili kwa mara ya kwanza Tanzania toka awe Rais wa  FIFA na alipokelewa na viongozi mbalimbali akiwemo Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dtk. Harrison Mwakyembe na Mwenyekiti wa Baraza la Michezo la Taifa Bw. Leodger Tenga na Rais wa TFF  Bw. Wallace Karia.


(mwisho)

IMETOLEWA NA:

OFISI YA WAZIRI MKUU,

ALHAMISI, FEBRUARI 22, 2018

Matangazo

  • TANGAZO LA UMILIKISHWAJI ARDHI February 13, 2021
  • Badili Tahasusi kwa Wanafunzi Kidato cha Tano Tarajali na Vyuo vya Kati April 01, 2021
  • SIS MOBILE APPLICATION April 01, 2021
  • TANGAZO LA AJIRA LEO 09 MEI,2021 May 09, 2021
  • Itizame yote

Habari mpya

  • MAPOKEZI YA FEDHA ZA MIRADI YA VITUO VYA AFYA VITATU (3) - 1,869,307,194 /=

    May 27, 2025
  • UJIO WA MADAKTARI BINGWA WA MHE. DKT. SAMIA SULUHU HASSAN, HOSPITALI YA WILAYA YA WANGING'OMBE

    May 20, 2025
  • TUZO ZATOLEWA KWA WAKIMBIZA MWENGE WA UHURU 2025, NGAZI YA WILAYA - WANGING'OMBE.

    May 16, 2025
  • VIJIJI 10 VYA WANGING'OMBE KUNUFAIKA NA HATI ZA KIMILA 3,010

    May 13, 2025
  • Itizame yote

Video

MAKALA YA MIAKA MIWILI YA RAIS SAMIA SULUHU HASSAN WILAYA YA WANGING'OMBE
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • Vivutio vya Utalii Wanging'ombe
  • Historia ya Halmashauri ya Wanging'ombe
  • Mfumo wa Mawasiliano ya ndani wa Serikali Government Mailing System (GMS)
  • Registration Of Allied Health Professionals
  • Mfumo wa maombi ya Ajira
  • baraza la taifa la elimu ya ufundi

Tovuti Mashuhuri

  • Mfumo wa Vibali vya Safari Nje ya Nchi kwa watumishi wanaopewa ruhusa na Katibu Mkuu Kiongozi
  • Mfumo wa Malalamiko na Pongezi
  • UTUMISHI
  • MFUMO WA SIS(SCHOOL INFORMATION SYSTEM)
  • TAMISEMI
  • BUNGE

Wasomaji mbalimbali duniani

world map hits counter

Idadi ya wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani

Copyright ©2021 Wanging'ombedc . All rights reserved.