Wananchi Wilayani Wanging'ombe wameagizwa kufanya usafi katika mazingira yao wanamoishi ili kuhakikisha mazingira yanakuwa safi na hivyo kuondokana na magonjwa yatokanayo na uchafu,Maagizo hayo yametolewa na Mhe Mkuu wa Wilaya Ndg Comrade Ally Kassinge wakati wa siku ya mazoezi kufuatia agizo la Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan yaliyofanyika katika Kijiji cha Igwachanya ambako ndio Makao Makuu ya Halmashauri tarehe 13/10/2018."Ninaagiza Wananchi wote katika Wilaya ya Wanging'ombe kufanya usafi katika mazingira wanayoishi ili tuweze kuepukana na magonjwa yanayosababishwa na uchafu wa mazingira" alisema Kassinge.
Aidha pamoja na kufanya mazoezi Mkuu wa Wilaya alifanya kazi ya kuzindua kikosi kazi cha kufanya usafi katika maeneo mbalimbali ndani ya Kijiji cha Igwachanya ili kufanya usafi kuwa endelevu,katika uzinduzi huo aliweza kugawa vifaa mbalimbali kwa ajili ya kuwawezesha kutekeleza majukumu hayo baadhi ya vifaa vilivyogawiwa ni pamoja na toroli,mavazi mifagio nk.Pia katika kuhamasisha wananchi kufanya mazoezi Mkuu wa Wilaya alizindua clabu ya wafanya mazoezi ambapo watakuwa wakifanya mazoezi hayo siku za jumamosi ,jumapili,na siku za mapumziko ya Kitaifa.
Siku hiyo iliambatana na madhimisho ya siku ya kifo cha Baba wa Taaifa Mwl Julius Kambarage Nyerere kwa kufanya mdahalo wenye maada "Miaka 19 bila Mwl Nyerere tumejifunza nini katika Elimu na Viwanda" Mdahalo huu uliendeshwa na wadau mbalimbali wakiwemo wataalamu na wanasiasa pamoja na wanafunzi wa ngazi zote kuanzia shule ya msingi hadi Sekondari kidato cha tano aidha wadau hao waliweza kuchangia kwa kuangalia sera za Mwl wakati wa uongozi wake na kufuatia awamu tofauti chini ya Marais tofautitofauti hadi hivi sasa tukiwa awamu ya Tano kwa ujumla wake awamu zote zimetekeleza kwa kadri ya uwezo wao lakini walisistiza kuwa awamu hii ya tano imejikita kwelikweli katika kuhakikisha elimu na viwanda vinaboreshwa na kuona kuwa awamu hii inaenenda sawasawa na nyendo za Mwl Nyerere.
Copyright ©2021 Wanging'ombedc . All rights reserved.