WANANCHI WAPOKEA VYEMA ZOEZI LA KUJIANDIKISHA DAFTARI LA WAPIGA KURA - WANGING'OMBE
Tarehe iliyowekwa: October 11th, 2024
Na. Nickson Kombe,
WANANCHI wa wilaya ya Wanging'ombe wamepokea vyema zoezi la kujiandikisha kwenye Daftari la Wapiga kura wakati wa Uzinduzi wa Zoezi hilo katika Kitongoji cha Wangama, kijiji cha Chalowe kata ya Igwachanya.
Akizindua Zoezi la Kujiandikisha katika Daftari la wapiga kura leo Oktoba 11, 2024, Mkuu wa wilaya ya Wanging'ombe, Mhe. Zakaria Saili Mwansasu ametumia fursa hiyo kuendelea kuhamasisha na kutoa elimu dhidi ya zoezi hilo namna ambavyo limekuwa ni la muhimu kuelekea Uchaguzi wa Serikali za mitaa 2024 na maendeleo ya jamii katika upatikanaji wa viongozi bora.
Hata hivyo katika Uzinduzi wa zoezi hilo, ambapo linafanyika katika vitongoji 525 vya wilaya ya Wanging'ombe limepokelewa vyema na wananchi wamehamasika sana jambo ambalo limepelekea kufanikiwa kwa asilimia 22 kufikia leo kuu la kuandikisha wapiga kura 112,792 wilaya yote.
Aidha Viongozi ngazi ya wilaya, kata na vitongoji wametumia nafasi hiyo kuwahimiza wananchi kuendelea kutumia haki yao ya msingi kuhakikisha wale wenye vigezo vya kujiandikisha kwenye daftari la wapiga kura, wanajitokeza kwa wingi kujiandikisha ili ifikapo tarehe 27 Novemba 2024 waweze kuwachagua Viongozi wanaowataka
Ikumbukwe kuwa zoezi la Uandikishaji kwenye Daftari la Wapiga Kura litafanyika kwa muda wa siku 10 kuanzia leo tarehe 11 hadi 20 Oktoba 2024.