Wananchi wilayani Wanging'ombe mkoani Njombe wametakiwa kuuenzi muungano kwa kudumisha amani na Upendo baina yao ili kuepuka migogoro isiyo ya lazima.
Rai hiyo imetolewa na mkuu wa wilaya ya wanging'ombe Ally Kassingewakati wa maadhimisho ya miaka 54 ya muungano wa Tanganyika naZanzibar yaliyofanyika Kijiji
cha Ilembula ambapo alisema ni vemawakaitunza amani ambayo ni tunu ya taifa.
"Tuuenzi muungano wetu kwa kuitunza amani tuliyonayo kwa faida ya familia na jamii zetu kwa ujumla"alisema Kassinge.Hata hivyo katika maadhimisho hayo pia mkuu
wa wilaya huyo alizindua chanjo ya saratani ya mlango wa kizazi ambapo alisema zaidi ya wasichana 1000 wanatarajiwa kupatiwa chanjo hiyo.Ambapo Mganga Mkuu
wa Wilaya alitumia fursa hiyo kuwaomba viongozi katika ngazi mbalibali wawahamasishe wananchi wao k kuwatoa wasichana wenye umri wa miaka 14 ili wapate
chanjo hiyo ambayo nisalama haina madhara. Alisema walengwa wakubwa wa chanjo hiyo ni wasichana hivyo kuwaasa wazazi kuwaeleza wabinti zao ili kufika katika
vituo na kupatiwa chanjo hiyo.
"Serikali imeamua kutoa chanjo hii ili kuwanusuru wasichana hawa ili kuepukana na athari zinazogharimu maisha ya wakinamama wengi"alisemaKassinge.Kwa upande
wa mganga mkuu wa halmashauri ya wilaya ya wangingombeJames Ligwa,alisema zaidi ya wanawake 500 wamepimwa kwa kipindi cha
miezi minne ambapo 50 kati yao wamegundulika kuwa na dalili za awali za saratani ya mlango wa kizazi. .
Copyright ©2021 Wanging'ombedc . All rights reserved.