UTEUZI WA WAGOMBEA UBUNGE JIMBO LA WANGING’OMBE KUPITIA VYAMA VYA CCM NA CHAUMMA.
Tarehe iliyowekwa: August 27th, 2025
UREJESHAJI wa fomu umekamilika leo tarehe 27 Agosti 2025 katika ofisi za Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, jimbo la Wanging’ombe, wagombea kupitia tiketi za CCM na CHAUMMA wameteuliwa kuingia kwenye kinyang’anyiro cha Uchaguzi mkuu 2025 unaotarajiwa kufanyika tarehe 29 Oktoba 2025.
Msimamizi wa Uchaguzi, Jimbo la Wanging’ombe, Bw. Mkali Kubebeka ameyasema hayo baada kupokea fomu za wagombea, kujiridhisha na kuwateuwa rasmi kuingia kwenye kinyang’anyiro cha Uchaguzi Mkuu 2025.
Kwa hivyo mgombea ubunge kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Jimbo la Wanging’ombe, Dkt. Festo Dugange amefanikiwa kurejesha fomu na kupata uteuzi rasmi.
Vivyo hivyo pia kwa mgombea wa ubunge kupitia Chama cha Ukombozi kwa Umma (CHAUMMA), Jimbo la Wanging’ombe, Bi. Faraja Mgimba amefanikisha kurejesha fomu na kupata uteuzi rasmi.
Aidha urejeshaji wa fomu umefanyika pia ngazi za kata na kuwepo kwa mafanikio tele kwa asilimia kubwa ya wagombea wa udiwani kupitia vyama vyao kuteuliwa kushiriki kinyang’anyiro cha Uchaguzi mkuu 2025.