TAMASHA LA UTAMADUNI NA USIMIKWAJI WA CHIFU KABILA LA WABENA - NYUMBANITU
Tarehe iliyowekwa: November 7th, 2023
Na Mwandishi Wetu,
Nickson Kombe,
Matukio ya kuadhimisha Tamasha la Utamaduni wetu "Tamaduni Festival" yakiambatana na Sherehe za Usimikwaji Chifu wa Kabila la Wabena, Kijiji cha Nyumbanitu, Kata ya Igima, Wanging'ombe.
Akialikwa Mgeni Rasmi, Mkuu wa Wilaya, Wanging'ombe, Mhe. Claudia Kitta amesema inatupasa kuheshimu tamaduni zetu na kuachana na mila potofu, utunzwaji wa mazingira na uhifadhi wa misitu ya asili ambapo itachangia pato la taifa na kutuletea fedha za kigeni kupitia kiwanda cha Utalii.
Mhe. Claudia ameongeza kwa kusema Serikali inatambua umuhimu wa misitu ya asili ikiwemo "Nyumbanitu" ikiwa na maana "Nyumbanyeusi". Serikali ya Awamu ya Sita itaendelea kuhakikisha maeneo hayo ambayo yamekuwa yakitumika kwa shughuli mbalimbali za mila kutunzwa na kuhifadhiwa kwa ajili ya utalii na vizazi vijavyo.
Sherehe za kusimikwa Chifu wa Kabila la Wabena ambaye ni wa awamu ya 9, anaitwa Bw. Charles Msambila Mkongwa zimeambatana na ngoma za asili, kutembelea msitu wa Nyumbanitu, mapango ya asili, nyimbo na ngonjera.
Aidha Chifu Mkongwa amewaasa wabena na waalikwa wote kuachana na mila potovu pale ambapo unaona watu wanaafanya maendeleo basi inawapasa kuwa na wivu wa kimaendeleo ambao ni mzuri kwa ustawi na sio kuwarudisha nyuma kimaendeleo.
Hata hivyo wananchi wa kijiji cha Nyumbanitu wanawakaribisha watalii wa ndani na nje ya nchi.