OPERESHENI YA KWANZA HOSPITALI YA WILAYA - WANGING'OMBE
Tarehe iliyowekwa: November 2nd, 2023
Na Mwandishi Wetu,
Rukia Omary,
Mganga Mkuu, Wilaya, Dkt. Frank Chiduo ameongoza jopo la Madaktari, Wauguzi na Wataalamu wa Usingizi kufanya operesheni ya uzalishaji kwa mara ya kwanza katika Hospitali ya Wilaya ya Wanging'ombe iliyopo Kijiji cha Ihanja, Kata ya Mdandu.
Daktari Frank amesema tangu uanzishwaji wa Hospitali hiyo mwaka 2020, huduma ya operesheni ya uzalishaji imeanza kutolewa rasmi leo kwa mafanikio makubwa "ni jambo la kumshukuru Mungu...huku Afya ya Mama na Mtoto ni njema". Hivyo wananchi wa Wanging'ombe hawana budi kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kutokana na juhudi zake za uboreshaji wa huduma za afya Wilaya ya Wanging'ombe.
Aidha uanzishwaji wa huduma ya operesheni ya uzalishaji katika Hospitali ya Wilaya ya Wanging'ombe iliyopo kijiji cha Ihanja, Kata ya Mdandu itampunguzia mgonjwa/mama mjamzito changamoto ya umbali iliyokuwepo awali, ambapo ilimlazimu mgonjwa kusafiri umbali mrefu kupata huduma hiyo.