• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe za watumishi |
Wanging'ombe District Council
Wanging'ombe District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Wanging'ombe

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati ya Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Kilimo
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii
      • Idara ya Mipango na Ufuatiliaji
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara ya Ujenzi
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Mazingira
      • Idara ya Ardhi na Maliasili
      • Utawala na Rasilimali Watu
    • Kitengo
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Manunuzi na Ugavi
      • Kitengo cha Nyuki
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Uchaguzi
      • Mawasiliano Serikalini
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Huduma
    • Huduma ya Maji
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha uongozi na Mipango
      • Kamati ya UKIMWI
      • Maadili
      • Uchumi,Afya na Elimu
    • Orodha ya Madiwani
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kumwona Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Miongozo
    • Fomu za Maombi
    • Gazeti la Serikali
    • Sheria ndogo za Halmashauri
    • Mpango mkakati wa Halmashauri
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Matukio
    • Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Hotuba

NAIBU WAZIRI TAMISEMI DR DUGANGE ATOA WITO KWA WATUMISHI WA AFYA NCHINI KUFANYA KAZI KWA KUZUNGATIA MAADILI

Tarehe iliyowekwa: April 10th, 2021

 *Na Maiko Luoga Wanging'ombe*

Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI Dkt, Festo Dugange ametoa wito kwa Watumishi wa Afya nchini kufanya kazi kwa kuzingatia Taratibu, nidhamu na maadili ya kutoa huduma kwa Wananchi wanaofika kwenye Vituo vya Afya kufuata matibabu.

Ametoa wito huo April 10, 2021 wakati akizungumza na Wananchi wa Kijiji cha Wangutwa Kata ya Uhambule Wilayani Wanging’ombe Mkoa wa Njombe alipofanya ziara ya kikazi kama Mbunge wa Jimbo la Wanging’ombe kwa lengo la kusikiliza kero za Wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.

Akiwa kwenye Mkutano wa hadhara Wananchi wa Kijiji hicho walimpa kero kuwa Watumishi wa Afya wanaofanya kazi katika Zahanati ya Kijiji chao mara nyingi hawapatikani kwenye Kituo cha kazi, kutoa lugha mbaya kwa Wagonjwa na kuto toa huduma za haraka huku wakisema hadi wamalize ratiba zao.

“Kwakweli Daktari aliopo hapa na Manesi wengine hawana mahusiano mazuri na Uongozi wa Kijiji, wao wanasema mwenye uwezo wa kuzungumza nao ni yule aliye waajiri sio sisi wa huku Kijijini, kuna wakati tumepoteza Watu wawili hapa kwa kukosa huduma za haraka, Nesi anasema anakula kwanza ndio aje kutibu” alisema Bw, Salumu Ngella Mwenyekiti wa Kijiji cha Wangutwa kwa niaba ya Wananchi.

Kufuatia kero hiyo ya Wananchi kwa Watumishi wa Sekta ya Afya Dkt, Festo Dugange ameahidi kuifanyia kazi na kuchukua hatua za kinidhamu kwa Watumishi watakaobainika kukiuka Taratibu za utumishi wa Umma huku akitoa maagizo kwa Waganga Wakuu wa Wilaya na Mikoa kote nchini kuwasimamia Waganga wa chini ili watoe huduma bora kwa Wananchi.

“Mimi nimelichukua hili, kunatatizo kubwa la kusimamia Watendaji wetu, sio wote wabaya lakini tatizo lipo kwenye usimamizi kote nchini tutachukua hatua za kinidhamu kwa kuzingatia Sheria kwa wote wanaofanya mchezo na Afya za Wananchi, pia natoa wito kwa Waganga Wakuu wa Halmashauri na Mikoa kuwasimamia Watumishi wa Vituo ili watoe huduma sahihi kwa Wananchi” alisema Dkt, Festo Dugange (MB) Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI.

Mhe, Dkt, Festo Dugange April 10, 2021 alifanya mikutano na Wananchi wa Vijiji vya Wangutwa Kata ya Uhambule, Mtapa na Igwachanya Kata ya Igwachanya Wilayani Wanging’ombe akisikiliza kero zao kama Mbunge wa Jimbo na kuzitafutia ufumbuzi, huku Wananchi wa maeneo hayo wakipongeza jitihada za Mbunge wao.

Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI HALMASHAURI YA WILAYA YA WANGING'OMBE 31 JULAI 2024 July 31, 2024
  • KUITWA KWENYE USAIL September 27, 2024
  • KUITWA KWENYE USAILI September 27, 2024
  • TANGAZO LA UMILIKISHWAJI ARDHI February 13, 2021
  • Itizame yote

Habari mpya

  • TUZO ZATOLEWA KWA WAKIMBIZA MWENGE WA UHURU 2025, NGAZI YA WILAYA - WANGING'OMBE.

    May 16, 2025
  • VIJIJI 10 VYA WANGING'OMBE KUNUFAIKA NA HATI ZA KIMILA 3,010

    May 13, 2025
  • BARAZA LA WAHESHIMIWA MADIWANI ROBO YA PILI YA MWAKA 2024/2025

    January 29, 2025
  • HERI YA SIKU YA KUZALIWA, MKURUGENZI MTENDAJI, DKT. PETER MAIGA NYANJA

    January 28, 2025
  • Itizame yote

Video

MAKALA YA MIAKA MIWILI YA RAIS SAMIA SULUHU HASSAN WILAYA YA WANGING'OMBE
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • Vivutio vya Utalii Wanging'ombe
  • Historia ya Halmashauri ya Wanging'ombe
  • Mfumo wa Mawasiliano ya ndani wa Serikali Government Mailing System (GMS)
  • Registration Of Allied Health Professionals
  • Mfumo wa maombi ya Ajira
  • baraza la taifa la elimu ya ufundi

Tovuti Mashuhuri

  • Mfumo wa Vibali vya Safari Nje ya Nchi kwa watumishi wanaopewa ruhusa na Katibu Mkuu Kiongozi
  • Mfumo wa Malalamiko na Pongezi
  • UTUMISHI
  • MFUMO WA SIS(SCHOOL INFORMATION SYSTEM)
  • TAMISEMI
  • BUNGE

Wasomaji mbalimbali duniani

world map hits counter

Idadi ya wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani

Copyright ©2021 Wanging'ombedc . All rights reserved.