Kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa Ndg Charles Francis Kabeho amepongeza miradi iliyokaguliwa na Mwenge wa Uhuru katika Wilaya ya Wanging’ombe kuwa ni ya kiwango kinachoendana na thamani ya fedha, aliyasema hayo terehe 29/05/2018 katika kijiji cha Imalinyi alipokuwa akikagua mradi wa barabara ya estate namba 5 masilu.
“Naridhia kuweka jiwe la ukaguzi wa ujenzi wa barabara hii kwa kuwa nimeridhika na namna ambavyo Mkandarasi amefanya kazi vizuri pamoja na wahandisi wanaosimamia mradi”alisema Ndg Kabeho.
Aidha Kiongozi wa Mbio za Mwenge alipongeza ujenzi wa madarasa matatu,bweni,choo aliofungua katika shule ya sekondari Wanike na ujenzi unaoendelea katika Kituo cha Afya Wanging’ombe ameomba salamu za pongezi ziwafikie wale wanaotengeneza Tofari kwani ni za viwango.
Wakati Mwenge wa Uhuru ukikimbizwa Mkuu wa Wilaya Comred Ally Kasinge alimuhakikishia Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa kuwa atasimamia yale yote aliyoshauri na kuagiza kwa dosari mbalimbali zilizoonekana katika miradi atahakikisha zinarekebishwa.
Aidha ujumbe wa mwenge Mwaka 2018 umefikishwa vizuri kwa wananchi wa Wilaya ya Wanging’ombe ukiwa na kauli mbiu “Elimu ni Ufunguo wa Maisha Wekeza Sasa kwa maendeleo ya Taifa Letu” pamoja na kauli mbiu hii Mbio za Mwenge wa Uhuru zimehamasisha wananchi wa Wilaya ya Wanging’ombe kuendeleza Mapambano dhidi ya Rushwa,VVU/UKIMWI, Matumizi ya madawa ya kulevya na mapambano dhidi ya Malaria.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa ameendelea kutoa pongezi za dhati kwa Uongozi wa Wilaya na Halmashauri kwa ujumla kwa namna ambavyo wamepokea Mwenge kwani kila walipopita wananchi walijitokeza kwa wingi kuulaki Mwenge wa Uhuru “Ingekuwa ni amri yetu tungeamua kubaki Wanging’ombe kwa kuwa Mlitupokea Vizuri na Kutukarimu” alisema Ndg Kabeho.
Copyright ©2021 Wanging'ombedc . All rights reserved.