KATIBU Tawala, Mkoa wa Njombe, Bi. Judica Omary (Kulia Pichani) akiambatana na Katibu Tawala, Wilaya Wanging'ombe, Bi. Veronica Gerald (Kushoto Pichani) pamoja na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji, Wakili Joshua Sanga (Katikati Pichani) wakihoji namna gani mashine za kilimo zinaweza kurahisisha kazi na kupata mazao mengi zaidi katika Maonyesho ya Sikukuu ya Wakulima (Nanenane) katika Mikoa ya Nyanda za Juu Kusini yanayofanyika katika Viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya.