MKUU wa Mkoa wa Njombe, Mhe. Anthony Mtaka (Kushoto Pichani) akiambatana na Mkuu wa Wilaya ya Wanging'ombe, Mhe. Zakaria Mwansasu (Katikati Pichani) wametembelea na kukagua baadhi ya mabanda katika Maonyesho ya Sikukuu ya Wakulima (Nanenane) katika Mikoa ya Nyanda za Juu Kusini yanayofanyika katika Viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya.