AFISA Kilimo, Wanging'ombe, Bw. Patience Pius Chawala (Kitengo cha Horticulture) akielezea umuhimu wa kufanya tafiti za kiwango cha tindikali (soil pH Scale Status) kwenye udongo ili kufahamu ni aina gani na kiwango gani cha mboleo kinahitajika ili kupata matokeo mazuri ya mazao, karibuni sana.
Pamoja na timu husika ya wataalamu wapo tayari kuhakikisha unapata uelewa wa kutosha na huduma nyinginezo husika, karibuni nyote BANDA letu linapatikana Geti la Mashariki barabara ya kutokea Uwanjani, Viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya.