MKUU wa Divisheni/Idara ya Elimu Msingi na Awali, Wanging'ombe, Bw. Zuberi Karugutu (Kushoto Pichani) akiendelea kujiandikisha baada ya kununua Unga bora wa lishe, unaotengenezwa na Kikundi cha Wakinamama, kata ya Ilembula kwa uwezeshwaji wa mikopo ya Asilimia 10 itokanayo na mapato ya Halmashauri inayosimamia na Idara ya Maendeleo ya Jamii, Wanging'ombe.