MAKUBALIANO MPANGO WA UJENZI SHULE MBILI ZA SEKONDARI KWA AWAMU KATA YA IGIMA
Tarehe iliyowekwa: October 18th, 2023
Na. Nickson Kombe,
18 Oktoba 2023.
Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango (KFUM) wakiambatana na wawakilishi kutoka Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Wanging'ombe wameridhia mpango wa Ujenzi Shule mbili za Sekondari Kata ya Igima utakaotekelezwa kwenye vijiji viwili ambavyo ni Nyumbanitu na Lusisi.
Akitoa mrejesho mara baada ya kusomewa taarifa ya Kamati ya Maendeleo ya Kata (KAMAKA) Igima, Mwenyekiti wa Kamati ya Ujenzi, Uongozi na Mipango (KFUM), Mhe. Onesmo Lyandala amesema kutokana na sababu za kijiografia, idadi ya wanafunzi na utayari wa wananchi wa kata ya Igima hamna budi kutekeleza mpango wa ujenzi wa Shule mbili za Sekondari kwa awamu katika vijiji vya "Nyumbanitu" na "Lusisi".
Akifafanua zaidi kuhusiana na utaratibu utakaotumika kutekeleza mpango huo, Mkurugenzi Mtendaji, Wilaya ya Wanging'ombe, Bi. Maryam Muhaji amesema atatoa ushirikiano pale ambapo KAMATA watahitaji ushauri wa wataalamu mbalimbali kipindi cha ujenzi ili ujenzi wa Shule hizo uweze kukidhi vigezo vya usajili unaoratibiwa na mamlaka za usimamizi wa ubora Sekta ya Elimu. Mpango wa Ujenzi Shule ya Sekondari Kata ya Igima imezidiwa na idadi ya wanafunzi haswa wanaojiunga kidato cha Kwanza na kupelekea uhitaji wa ongezeko la Shule ya Sekondari Kata ya Igima.
Hata hivyo mara baada ya wajumbe wa Kamati ya Maendeleo Kata (KAMAKA) kushindwa kukubaliana ni kijiji kipi kati ya "Nyumbanitu" au "Lusisi" ujenzi huo utekelezwe. Waliamua kuwashirikisha wataalamu kutoka Halmashauri kufanya ukaguzi wa maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya ujenzi wa Shule ya Sekondari iwapo yamekidhi vigezo, na ndipo wataalamu kurejesha sababu za kuchagua kijiji cha "Nyumbanitu", Akitolea ufafanuzi wa changamoto mbalimbali walizopitia awali, Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Diwani Kata ya Igima, Bi. Paulina Samata.
Wawakilishi kutoka Ofisi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Wanging'ombe wamesisitiza dhidi ya ushirikiano baina ya wajumbe wa KAMAKA ili kufanikisha utekelezwaji miradi ya mpango wa ujenzi wa Shule mbili za Sekondari Kata ya Igima.
Aidha Wajumbe wa KAMAKA, Igima wametoa neno la shukrani kwa usuluhishi wa mgogoro huo.