Na
Veronica Keneth
Katika kuadhimisha miaka 60, ya Uhuru wa Tanganyika,Mkoa wa Njombe uliteua Wilaya ya Wanging′ombe kuwa mwenyeji wa Maadhimisho hayo ambapo Mgeni rasmi alikuwa Mhe Mkuu wa Mkoa wa Njombe Marwa Lubirya.Kumeku
kuwa na mafanikio mengi katika Nchi yetu Mkoa wetu na Wilaya zetu tangu nchi hii ilivyopata Uhuru nawaomba wananchi wenzangu tuyaenzi mafaniko haya kwa kuendelea kufanya kazi kwa bidii na kudumisha Amani yetu alisema Mkuu wa Mkoa, ameyasema hayo
wakati wa Maadhimisho ya Miaka 60 ya Uhuru wa Tnganyika yenye kauli mbiu
“Miaka 60 ya Uhuru Tanzania imara Kazi iendelee″ yaliyofanyika Kimkoa katika Wilaya ya Wanging'ombe maadhimisho hayo yamefanyika katika viwanja vya Hospitali ya Wilaya ambapo yaliambatana na Uwekaji wa Jiwe la Msingi katika Majengo ya Hospitali ya Wilaya y
yaliyopo Katika Kijiji cha Ihanja leo tarehe 08/112/2021.
Akifungua Sherehe hizo Mhe Mkuu wa Wilaya ya Wanging'ombe Lautery John Kanoni alimshukuru Mkuu wa Mkoa kwa kuipa Heshima Wilaya yake kuwa Mwenyeji wa Maadhimisho hayo.Wilaya ya Wanging'ombe ni Wilaya changa kati ya Wilaya zote za Mkoa wa Njombe
pamoja na uchanga wake kuna mafanikio makubwa yaliyopatika tangu kuanzishwa kwake ikiwa ni Mafanikio katika sekta ya Elimu ambapo uandikishaji umeoongezeka,vyumba vya madarasa vimeongezeka,Idadi ya Walimu pia imeongezeka Sekta ya Afya pia kuna mabadiliko makubwa ikiwemo ongezeko la vituo vya kutolea Huduma za Afya ikiwemo hospitali hii ambayo leo umeweka jiwe la Msingi.
Secta ya Maji upatikanaji wa Maji pia Umeongezeka kwa kiasi kikubwa sana,Secta ya Barabara kumekuwa na Ongezeko la barabara nyingi zinazo wezesha Wananchi kusafirisha mazao yao bila shida yeyote,Secta ya Umeme ambapo kwa sasa takribani vijiji 100 vimefikishiwa Umeme na Mchakato wa kumalizia vijiji nane vilivyobaki unaendelea.Aliongeza kwa kusema Pia Halmashauri imeweza kuongeza wigo wa ukusnyaji Mapato toka Tsh 600,000,000/=
hadi Tsh 2,900,000,000/=
Maadhimisho hayo yamehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Mkoa wa Njombe wakiwemo Wakuu wa Wilaya zote,wakurugenzi,Makatibu tawala wa Wilaya
na Waheshimiwa Madiwani na Viongozi wa Chama cha Mapinduzi Mkoa na Wilaya.
Akihutubia Wananchi Mhe Mkuu wa Mkoa aliwakumbusha wananchi kuwa ili tuyaenzi mafanikio hayo na kuyafanya yawe na Mwendelezo ni lazima kuwa na Wanchi wenye afya Njema hivyo amewasihi wananchi kujitokeza kuchanja dhidi ya Ugonjwa wa Uviko-19 ambao kwa sasa kunatishio la wimbi la nne.
Pia amewakumbusha ili serikali iweze kugawa rasilimali zake bila ya upendeleo ni lazima ijue idadi ya Wananchi wake itakayokuwa inawahudumia hivyo amewasihi wananchi pia kujitokeza kuhesabiwa katika zoezi la Sensa ya Watu na Makazi itakayofanyika Mwakani mwezi wa nane.
Katika Maadhimisho hayo walitambuliwa wazee waliozaliwa tarehe 09/12/wakati wa uhuru na kuwalisha Keki iliyoandaliwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Wanging'ombe Bi Maryamu A Mhaji Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa Halmashauri imeandaa Keki ikiwa ni ishara ya kuenzi Yote Mazuri yaliyofanyika na Serikali tangu kupata Uhuru na kuheshimu jitihada za wazee wetu waliokuwepo tangu Uhuru alisema Mkurugenzi Mtendaji.
Viongozi wa CCM mkoa pia walipata fursa ya kutoa salamu za Miaka 60 ya uhuru ambapo katoibu wa CCM Mkoa aliweza kuwasalimu wananchi na kujitambulisha rasmi kuwa yeye ndie Katibu wa CCM wa Mkoa wa Njombe na amekuja kuktetea Chama ili kuiwezesha Serikali iliyoko Madarakani kutekeleza Ilani yake vizuri hivyo amewaomba wananchi kuchapa kazi.
Copyright ©2021 Wanging'ombedc . All rights reserved.