Na Mwandishi Amon Chalamila
Mwenyekiti wa kamati ya siasa Wilaya ya Wanging’ombe Ndg Frank Chaula amelipongeza baraza la madiwani na wataalamu wa Halmashauri ya Wilaya ya Wanging’ombe kwa usimamizi mzuri wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika Wilaya,ameyasema hayo Tarehe 26 -8-2024 wakati wa ziara ya ukaguzi wa Miradi iliyofanywa na kamati ya siasa ya Wilaya ya Wangingombe,Kamati ya siasa ilifanya ukaguzi wa miradi ya Afya katika Kata ya Ilembula ambapo mradi wa ujenzi wa Kituo cha Afya wenye thamani ya Tsh 500,000,000/-unatekelezwa,Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya iliyopo Kijiji cha Ihanja ambapo kamati ilikagua ujenzi wa jengo la upasuaji wanaume,Wodi la Wanaume na Jengo la kuhifadhia maiti pia kamati ilikagua mradi wa Ujenzi wa Zahanati ya Ng’anda,aidha katika ziara hiyo Pamoja na pongezi Kamati iliiagiza Serikali kupitia Mkuu wa Wilaya Bi Claudia Kitta kuhakikisha maboma yote yanatengewa fedha na kumalizia kwa sababu wananchi wameshatekeleza kwa kiasi kikubwa, maboma yaliyoelekezwa kumaliziwa ni Jengo la Wagonjwa wa nje Kituo cha Afya Ilembula na Jengo la nyumba ya Watumishi Zahanati ya Ng’anda.” Wananchi wamefanya kazi kubwa kujenga maboma haya sasa si vema nguvu za wananchi zikapotea bure naagiza serikali kupitia Mkuu wa Wilaya kuielekeza Halmashauri kutenga fedha na kumalizia maboma haya ili wananchi wasione kama serikali yao imewatupa na kushindwa kuwaunga mkono katika jitihada zao za kujiletea maendeleo pia hili ni agizo la Mhe Waziri Mkuu hivyo mnapaswa kutekeleza mara moja” alisema Mhe Mwenyekiti waCCM Wilaya.Aidha Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya Bi Claudia Kitta alikiri kupokea maelekezo hayo ya Chama na Kuahidi kulifanyia kazi kwa haraka.Katika Ziara hiyo Pia Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya Bi Agnetha Mpangile alishiriki huku akiahidi kuyafanyia kazi maelekezo ya Chama kwa Kuwasilisha katika Vikao vya Halmashauri na kufanyia maaamuzi.Katika Ziara hiyo Kamati ya Siasa walitembelea pia Soko la Igula ambapo wakala wa Chakula NFRA wananunua mahindi kutoka maeneo mbalimbali ya Wilaya, amabapo baada ya kufika eneo la soko la Igula kamati iliweza kukutana na wakulima wanaopeleka mazao yao na kuwaelekeza Wawakilishi wa NFRA kuhakikisha wanaongeza kasi ya upimaji mahindi na kuondoa foleni kubwa iliyopo “Tumepata taarifa kuwa kuna viashiria vya rushwa katika kununua mahindi ambapo wakulima hawapewi kipaumbele na badala yake mnawapa kipaumbele wafanyabiashara sasa tunaomba mbadilike ikiwa nipamoja na kuongeza mizani na vitendea kazi vingine” alisema Mhe Mwenyekiti wa CCM Wilaya.Aidha Mheshimiwa Mwenyekiti wa Halmashauri Bi Agnetha Mpangile aliwasisitiza wananchi kuzingatia sheria kanuni na taratibu za Halmashauri kwa kuhakikisha wanalipa mapato ya Halmashauri.Aidha Mkuu wa Wilaya amesisitiza Wakulima kuhakikisha wanakuwa na barua inayowatambulisha kuwa ni wakulima kutoka katika vijiji wanakulima pale wanaposafirisha mazao yao vinginevyo wanapaswa kulipa ushuru wa Halmashauri ambao ndio unasaidia kutekeleza miradi ya maendeleo mbalimbali katika Wilaya” Hapa nisistize Sheria za Halmashauri zinakutaka kulipa ushuru pale unapokuwa umefanya biashara hivyo kama wewe ni Mkulima na unasafirisha mazao yako kupeleka NFRA hakikisha unapewa barua ya utambulisho kuwa ni mkulima na sio mfanyabiashara kwa sababu ni vigumu kubaini mkulima ni yupi na Mfanyabiashara ni yupi vinginevyo kama huna Barua ya utambulisho utapaswa kulipa Ushuru” alisema Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya.Aidha Kamati imepongeza na kuwaomba wananchi waiamini serikali yao ya awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe Daktari Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa CCM Taifa kwa kuendelea kufanya kazi kwa bididi ili kuliletea Taifa Maendeleo.
Copyright ©2021 Wanging'ombedc . All rights reserved.