Halmashauri ya Wilaya ya Wanging’ombe imepongezwa kwa kutekeleza vizuri mradi wa Ujenzi wa Vyumba 51 vya madarasa kupitia Mradi Na.5441 TCRP.Pongezi hizo zimetolewa na Katibu Tawala Wa Mkoa Bi Judika Omary leo tarehe 23/12/2021 katika Halmashauri ya Wilaya ya Wanging’ombe alipokuwa katika ziara ya Ukaguzi wa Miradi
”Kipekee nichukue fursa hii kuwapongeza Mkuu wa Wilaya,Mkurugenzi Mtendaji, Wakuu wa Idara,Watumishi wote kuanzia ngazi ya Kata hadi vijiji pamoja na wananchi wote kwa kazi kubwa na nzuri mliyoifanya kwani naamini bila ushirikiano huo kazi hii ingekuwa bado sana niwaombe mdumishe ushirikiano huu kwa miradi yote itakayoendelea kuja”. Alisema Katibu Tawala.
Aidha Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Wanging’ombe Bi Maryam Muhaji amesema kwa asilimia 99 mradi umekamilika mambo yaliyobaki ni madogo madogo ikiwemo kupanga madawati kufanya usafi wa maeneo ya ujenzi alimuhakikishia Katibu Tawala kuwa amepokea maelekezo yote na atayafanyia kazi na kuhakikisha Madarasa yote yanakamilika kabla ya Tarehe 31/12/2021 ambayo ni siku ya mwisho Kitaifa ya Kukabidhi Mradi huo."Nipende kukushukuru Katibu Tawala kwa Ziara yako napokea ushauri wote ulioutoa na kuufanyia kazi ili kuhakikisha Madarasa haya yanakamilika kabla ya tarehe 31/12/2021 ili ifikapo januari 2022 watoto wetu waweze kutumia vyumba hivi kama ilivyo nia ya Serikali".Alisema Mkurugenzi
Copyright ©2021 Wanging'ombedc . All rights reserved.