FOMU ZA UTEUZI MGOMBEA KITI CHA UBUNGE ZATOLEWA JIMBO LA WANGING'OMBE.
Tarehe iliyowekwa: August 25th, 2025
WAGOMBEA wa Ubunge Jimbo la Wanging’ombe kupitia vyama vya Chama cha Mapinduzi (CCM) na Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA), vikiwakilishwa na Dkt. Festo Dugange (CCM) na Bi. Faraja Mgimba (CHAUMMA) leo Jumatatu Agosti 25, 2025 wamechukua fomu za uteuzi ubunge katika jimbo la Wanging’ombe kwa tiketi za vyama vyao.
Fomu hizo wamekabidhiwa na Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo la Wanging’ombe, Bw. Mkali Kubebeka na endapo watateuliwa na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) kugombea nafasi hizo, watawakilisha vyama vyao katika jimbo hilo.
Hata hivyo, zoezi la uchukuaji fomu za uteuzi katika Jimbo la Wanging’ombe limekamilika vyema na wanatarajia kuendelea na hatua nyinginezo.