Wizara ya Habari Mawasiliano na Teknolojia ya Habari (WMTH) kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi inatekeleza Mfumo wa Anwani za Makazi nchini.
Mfumo huu ni Muundombinu unaotambulisha mtu alipo, anapopatikana ama anapotakiwa kuhudumiwa (nyumbani, ofisini ama eneo la biashara).
Chimbuko la Anwani za Makazi ni Sera ya Taifa ya Posta ya mwaka 2003, Makubaliano ya Kimataifa (Pan African Postal Union(PAPU) na Universal Postal Union(UPU)) na Ilani ya Chama Cha Mmapinduzi (CCM) ya 2020 – 2025 kifungu Na. 61(m) zinazoelekeza kuhakikisha Anwani za Makazi zinawekwa nchini ili kurahisisha upatikanaji, utoaji na ufikishaji wa huduma katika maeneo mbalimbali.
•Anwani ya Makazi inaundwa na vitu vikuu vitatu ambavyo ni:
1. Namba ya Anwani (namba ya jengo/kiwanja)•
2. Jina la Barabara/Jina la Kitongoji/Shehia na•
3. Postikodi
•Namba ya Anwani inaweza kueleweka kama namba ya jengo/nyumba. Hata hivyo ni vyema kutumia “Namba ya Anwani” kwani baadhi ya anwani hazina majengo
.•Hii ni namba kamili inayoonekana mbele ya jengo kwenye kibao cha njano au iliyochorwa kwa karamu ya rangi kwenye ukuta wa nyumba, getini au mlangoni.
•Namba ya Anwani inaweza kueleweka kama namba ya jengo/nyumba. Hata hivyo ni vyema kutumia “Namba ya Anwani” kwani baadhi ya anwani hazina majengo.
Anwani ya Makazi inajumuisha taarifa za kijiografia, wamiliki na wategemezi wa Anwani, majengo yaliyopo kwenye Anwani na huduma mbalimbali zinazopatikana kwenye Anwani husika (mf. Shule, Zahanati n.k)
Copyright ©2021 Wanging'ombedc . All rights reserved.