ELIMU YA LISHE MTAMBUKA YATOLEWA KIJIJI CHA CHALOWE WILAYA YA WANGING’OMBE
Tarehe iliyowekwa: December 18th, 2023
Na. Mwandishi Wetu,
Rukia Omary,
Halmashauri ya wanging’ombe kupitia Idara ya Afya wanatekeleza mpango wa huduma za Lishe mtambuka mwaka wa fedha 2024/2025. Wataalamu wa Afya na Lishe wanaendelea kutoa Elimu ya Afya na Lishe Kijiji , utolewaji wa matone ya vitamini kwa Watoto Pamoja Upimaji wa virusi vya Ukimwi kwa Kwa kutumia vipimo vipya vinavyotumia ute wa mate kubaini maambukizi ya VVU katika vijiji na Kata na siku ya Lishe imefanyika katika Kijiji Cha Chalowe Wilaya ya Wanging'ombe.
Afisa lishe Wilaya ya Wanging’ombe Bi. Zenobia Aloyce amefafanua suala la lishe ni muhimu wazazi kutambua makundi ya vyakula vya lishe kuimarisha afya ya mtoto na akili na kujikinga dhidi ya magonjwa ya utapiamlo na udumavu. Akatilia mkazo kwa wazazi kuwanyonyesha Watoto maziwa kwa kipindi cha miaka miwili na kuepuka kuwapa vinywaji vilivyosindikwa isipokuwa watumie matunda ya asili yenye virutubisho asilia.
Daktari wa Wilaya ya Wanging’ombe Bw. Alidius Muhule akiambatana na Bi Salome Lwendo waliwaelimisha wananchi kupima virusi vya Ukimwi kwa kutumia vipimo vinavyotumia ute wa mate kubaini maambukizi endapo utaona dalili zenye viashiria vyenye maambukizi ya Ukimwi na kuwaelekeza namna ya kutumia vipimo hivyo. Pia wakatoa ushauri kwa wale watakaobainika kuwa na maambukizi wafike haraka katika vituo vya Afya au zahanati kupima tena ili kujiridhisha kama kweli kuna maambukizi na kuanzishiwa huduma za dawa za kufubaza virusi mapema wasichukue maamuzi ya kutumia dawa bila ushauri wa wataalamu.
Wananchi wa Kijiji cha Chalowe wameishukuru serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kwa kupambana kuhakikisha wanatokomeza udumavu na utapiamlo tutashirikiana na wataalamu wetu wa afya kupambana dhidi ya janga hili.