• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe za watumishi |
Wanging'ombe District Council
Wanging'ombe District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Wanging'ombe

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati ya Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Kilimo
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii
      • Idara ya Mipango na Ufuatiliaji
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara ya Ujenzi
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Mazingira
      • Idara ya Ardhi na Maliasili
      • Utawala na Rasilimali Watu
    • Kitengo
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Manunuzi na Ugavi
      • Kitengo cha Nyuki
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Uchaguzi
      • Mawasiliano Serikalini
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Huduma
    • Huduma ya Maji
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha uongozi na Mipango
      • Kamati ya UKIMWI
      • Maadili
      • Uchumi,Afya na Elimu
    • Orodha ya Madiwani
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kumwona Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Miongozo
    • Fomu za Maombi
    • Gazeti la Serikali
    • Sheria ndogo za Halmashauri
    • Mpango mkakati wa Halmashauri
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Matukio
    • Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Hotuba

BALOZI WA MAZINGIRA AMEWAASA WANANCHI KUJENGA UTAMADUNI WA KUPANDA MITI YA MATUNDA - WANGING’OMBE

Tarehe iliyowekwa: October 8th, 2023

Na. Mwandishi Wetu,
Rukia Omary,


Balozi wa mazingira, Aihdi Sinene akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Wanging’ombe, Mheshimiwa Claudia Kitta wamepanda miti ya matunda Parachichi aina ya Hasi katika Shule ya msingi mpya Igwachanya iliyojengwa kupitia mradi wa  BOOST.

Katika Ziara hiyo, Balozi wa Mazingira na msafara wote wamefanikiwa kupanda miche 20 ya Parachichi aina ya Hasi, Miche hiyo imepandwa katika viunga vya shule mpya ya msingi Igwachanya iliyojengwa kupitia mradi wa  BOOST, Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Wanging’ombe, Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji.


Akihutubia wananchi wa Kata ya Igwachanya, Balozi wa Mazingira, Aihdi Sinene  amenukuu kauli mbiu ya “Tunza mazingira Yakutunze” ikiwa ni kampeni mahususi na muhimu kwa Maisha ya viumbe hai, pia ameongelea umuhimu wa upandaji miti ya matunda kutekekeleza sera ya mazingira, afya, lishe na kupunguza athari za mabadiliko ya tabia nchi na kuepuka kukata miti ovyo. Ujumbe huu wa mazingira ulianzishwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan hapo awali akiwa ni Makamu wa Rais katika Serikali ya awamu ya tano Makutopora jijini Dodoma na sera hii inaendelea kutekelezwa ili kudumisha utamaduni wa upandaji miti.


Mkuu wa Wilaya ya Wanging’ombe, Mhe. Claudia Kitta amesema utamaduni wa kupanda miti ya matunda kama parachichi na matunda mengineyo ya asili yanachangia kupunguza matatizo ya utapia mlo kwa Watoto na baadhi ya aina za matunda hayo yanaweza kuongeza vipato vya wananchi. Hivyo amewaasa wananchi wa Wilaya ya Wanging’ombe kuendelea kupanda miti ya matunda majumbani na taasisi za Umma kwa kufuata taratibu za kitaalamu ili kuleta tija katika jamii na taifa kwa ujumla.


Aidha Balozi wa Mazingira, Aihdi Sinene amesema suala la upandaji miti ni la Kitaifa kila mwananchi anawajibu wa kupanda miti kwani husaidia kutunza vyanzo vya maji na kuzuia mmomonyoko wa ardhi na kuifanya jiografia ya mazingira kuwa bora Zaidi. Ameyasema hayo akiwa ameongozana na Mhe. Mkuu wa Wilaya, Katibu Tawala, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri, Katibu wa Wazazi  CCM. Mapinduzi, Afisa Elimu Kata, Mwalimu Mkuu S/M Igwachanya na wajumbe wengineyo.



Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI ZA MUDA ZA WATENDAJI WA VITUO VYA KUPIGIA KURA KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2025 June 28, 2025
  • TANGAZO LA KAZI, HALMASHAURI YA WILAYA YA WANGING'OMBE August 19, 2025
  • TANGAZO LA UMILIKISHWAJI ARDHI February 13, 2021
  • Badili Tahasusi kwa Wanafunzi Kidato cha Tano Tarajali na Vyuo vya Kati April 01, 2021
  • Itizame yote

Habari mpya

  • UTEUZI WA WAGOMBEA UBUNGE JIMBO LA WANGING’OMBE KUPITIA VYAMA VYA CCM NA CHAUMMA.

    August 27, 2025
  • MAAFISA MAENDELEO YA JAMII KUWEZESHWA VISHIKWAMBI 18 -WANGING’OMBE

    August 27, 2025
  • DC MWANSASU: “ZINGATIENI ELIMU BILA KUJALI UMRI”

    August 26, 2025
  • FOMU ZA UTEUZI MGOMBEA KITI CHA UBUNGE ZATOLEWA JIMBO LA WANGING'OMBE.

    August 25, 2025
  • Itizame yote

Video

MAKALA YA MIAKA MIWILI YA RAIS SAMIA SULUHU HASSAN WILAYA YA WANGING'OMBE
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • Vivutio vya Utalii Wanging'ombe
  • Historia ya Halmashauri ya Wanging'ombe
  • Mfumo wa Mawasiliano ya ndani wa Serikali Government Mailing System (GMS)
  • Registration Of Allied Health Professionals
  • Mfumo wa maombi ya Ajira
  • baraza la taifa la elimu ya ufundi

Tovuti Mashuhuri

  • Mfumo wa Vibali vya Safari Nje ya Nchi kwa watumishi wanaopewa ruhusa na Katibu Mkuu Kiongozi
  • Mfumo wa Malalamiko na Pongezi
  • UTUMISHI
  • MFUMO WA SIS(SCHOOL INFORMATION SYSTEM)
  • TAMISEMI
  • BUNGE

Wasomaji mbalimbali duniani

world map hits counter

Idadi ya wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani

Copyright ©2021 Wanging'ombedc . All rights reserved.