Serikali kupitia Mradi wa uimarishaji Mifumo katika Sekta za Umma inategemea kuzindua rasmi Tovuti za Mamlaka ya Serikali za Mitaa kwa Mikoa ya Njombe, Rukwa, Mbeya na Songwe tarehe 27 Machi 2017 tukio hilo litafanyika katika Ukumbi wa Tughimbe ulioko Jijini Mbeya.
Uzinduzi huo unafanyika baada ya mafunzo kwa Maafisa TEHAMA na Habari kukamilka tarehe 25 Machi 2017.