JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
OFISI YA RAIS
TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA
(Barua zote zitumwe kwa Mkurugenzi Mtendaji)
Unapojibu tafadhali taja:-
Kumb. Na. WDC/A.10/11/50 25 Februari, 2022
TANGAZO LA NAFASI YA KAZI YA KUKUSANYA TAARIFA ZA ANWANI YA MAKAZI NA POSTIKODI
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Wanging’ombe anapenda kuwatangazia nafasi 240 za ajira ya muda kwa nafasi za wakusanya taarifa kwenye zoezi la anwani za makazi katika kata na vijiji vyote vya Halmashauri ya Wilaya ya Wanging'ombe
SIFA ZA WAOMBAJI
Awe raia wa Tanzania mwenye umri kati ya miaka 18 – 34
Awe na elimu kuanzia kidato cha nne na kuendelea.
Awe anamiliki simu janja android kuanzia toleo la 8.10 yenye uwezo wa kukaa na chaji kwa siku nzima nauwezo wa kuhifadhi Taarifa kwa uwezo wa 32gb au zaidi.
Awe na uwezo wa kutumia program tumizi za Simu janja.
Awe na barua pepe (email address) na nywila (password) inayofanya kazi
Awe ana uwezo wa kusoma ramani za mitaa
Awe ni mkazi wa kata/kijiji husika
Awe na uwezo wa kufanya kazi kwa muda mrefu.
KAZI NA MAJUKUMU
Kugawa/kuandika namba za nyumba, viwanja na maeneo ya huduma
Kukusanya taarifa za nyummba, viwanja na maeneo ya huduma
Kukusanya taarifa za wamiliki wa nyumba, viwanja na maeneo ya huduma kwa kutumia mfumo wa anwani za makazi.
Kazi hii itafanyika kwa muda wa siku 20
MAOMBI YAAMBATANISHWE NA :
Nakala ya cheti cha kidato cha nne na kuendelea
Nakala ya cheti cha kuzaliwa
Picha (passport size 2)
Barua ya maombi ipite kwa mtendaji wa Kata anapoishi.
JINSI YA KUTUMA MAOMBI
Barua zote za maombi ziandikwe kwa mkono zikiwa na anwani kamili ya mwombaji, namba ya simu, barua pepe ziwasilishwe ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya kwa anwani ifuatayo:
MKURUGENZI MTENDAJI
HALMASHAURI YA WILAYA YA WANGING’OMBE
S.L.P 64
NJOMBE
TAREHE YA MWISHO KUPOKEA MAOMBI
Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 01/03/2022 saa 9:30 Alasiri.
Ferd Y Mhanze
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji
Halmashauri ya Wilaya ya Wanging’ombe
Barua zote zitumwe kwa Mkurugenz wa Halmashauri ya Wilaya ya Wanging’ombe, S. L. P. 64 Njombe, unaweza pia kuwasilianan nasi kwa Simu/Nukushi Na: +255026 2782111,
Tovuti: www.wangingombedc.go.tz, Barua pepe: ded@wangingombedc.go.tz
Copyright ©2021 Wanging'ombedc . All rights reserved.