JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni AHADI YA UADILIFU KWA SEKTA BINAFSI Kwa kutambua wajibu na nia njema ya Sekta Binafsi katika kuchangia kutokomeza rushwa kwa kuzingatia maadili, uwazi, na kutovumilia aina yoyote ya rushwa katika uendeshaji wa shughuli zote za biashara. Kwa kutambua wajibu wa kiuchumi, kimazingira, kijamii na manufaa mengine ya Taifa; kwa niaba ya Taasisi, Mimi........................................... ninaahidi kwa umma kwamba: 1. Tutashiriki kikamilifu kuchangia uchumi wa Taifa kwa njia ya kulipa kodi kutokana na shughuli zote za kibiashara kwa njia ya uwazi na uadilifu; 2. Hatutashawishi, kuomba, kupokea au kutoa hongo au aina yoyote ile ya rushwa; 3. Tutahakikisha kuwa mfumo wa kutoa taarifa za mapato ni wa wazi na kutoruhusu kamwe vitendo vya rushwa na utovu wa maadili katika manunuzi; 4. Tutahakikisha kuwa Kanuni za Maadili katika Taasisi yetu zinatufanya tuwajibike na kukuza mwenendo wa kimaadili ndani na nje ya mazingira ya biashara, na zitaendelea kuwa mwongozo kwa Menejimenti na Wafanyakazi kuwajibika kwa vitendo wakati wote; 5. Tutaepuka mazingira yote yanayoweza kusababisha mgongano wa kimaslahi na kuhakikisha kuwa tunatoa taarifa na kutatua masuala yote yenye migongano ya kimaslahi yanayojitokeza kwa njia ya uwazi na ufanisi; 6. Tutadumisha uwazi na ufanisi katika ngazi zote za Taasisi yetu na kutekeleza mfumo wetu wa udhibiti wa ndani ili kudumisha utawala bora na kujenga misingi ya uadilifu, uwajibikaji na uwazi katika shughuli zetu za biashara; 7. Tutahakikisha bidhaa na huduma zote tunazotoa zinazingatia viwango vya kitaifa na kimataifa; PL.5 8. Tutaweka taratibu za mawasiliano kwa njia ya siri ambazo zitahakikisha kuwa haki za wasambazaji, wateja na wafanyakazi zinalindwa na kuwanufaisha kwa kuhakikisha kuwa machapisho yanayohusu maadili mahali pa kazi yanakuwepo wakati wote ili kukuza ufahamu wao; 9. Tutakuwa raia wema na mfano mzuri wa kimaadili katika Taasisi na kushiriki kikamilifu kuhakikisha uwepo wa ustawi endelevu wa jamii, uchumi na hifadhi ya mazingira kwa kufanyakazi kwa mtazamo chanya ambao utaleta mabadiliko kwa Taifa zima. Tutahakikisha kuwa ushindani wa haki, uwazi na utawala bora katika shughuli zetu zote za kibiashara ni sehemu muhimu katika utamaduni wetu wa kufanyabiashara; Tutaepuka kushirikiana na makampuni ambayo yanakiuka maadili ya kibiashara; Tutaunga mkono uanzishaji wa programu za kuzuia na kupambana na rushwa na kushiriki katika kutumia nyenzo na mikakati iliyoanzishwa kwa lengo la kuhakikisha uwepo wa uwazi, ufanisi na uadilifu katika shughuli za biashara; Tutaunga mkono kampeni za mapambano dhidi ya rushwa duniani kote ambazo zinadumisha mazingira ya haki katika soko na kuimarisha Utawala Bora na uwazi katika shughuli zote za biashara. Hatutatoa, kuwezesha, kushawishi au kutoa zawadi kwa Afisa yeyote wa Umma, familia zao au washirika wao wa kikazi katika shughuli inayohusiana na mchakato wa manunuzi au katika utekelezaji wa mkataba; Tamko: Ninakiri kuwa nimesoma masharti yaliyomo katika Hati hii ya Ahadi ya Uadilifu na kuyaelewa kabla ya kuweka sahihi. Ninakubaliana na kutambua kwamba masharti yaliyomo katika Hati hii ni ya kisheria na ya kimaadili na ninawajibika kuyafuata. Pia, ninafahamu kuwa ukiukwaji wa masharti hayo ni uvunjaji wa Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa, Sheria ya Ununuzi wa Umma, Sheria ya Uhujumu Uchumi au Sheria nyengine za nchi na hatua za kisheria zinaweza kuchukuliwa dhidi yangu iwapo nitakiuka masharti hayo. ………………………………. ……………… …....………. …………….. JINA LA MTENDAJI MKUU KAMPUNI SAINI TAREHE Muhuri wa Kampuni ……………… ………………………… …………………… …………….. JINA LA MTENDAJI MKUU -BRELA SAINI TAREHE 10. 11. 12. 13. 14. 8. Tutaweka taratibu za mawasiliano kwa njia ya siri ambazo zitahakikisha kuwa haki za wasambazaji, wateja na wafanyakazi zinalindwa na kuwanufaisha kwa kuhakikisha kuwa machapisho yanayohusu maadili mahali pa kazi yanakuwepo wakati wote ili kukuza ufahamu wao; 9. Tutakuwa raia wema na mfano mzuri wa kimaadili katika Taasisi na kushiriki kikamilifu kuhakikisha uwepo wa ustawi endelevu wa jamii, uchumi na hifadhi ya mazingira kwa kufanyakazi kwa mtazamo chanya ambao utaleta mabadiliko kwa Taifa zima. Tutahakikisha kuwa ushindani wa haki, uwazi na utawala bora katika shughuli zetu zote za kibiashara ni sehemu muhimu katika utamaduni wetu wa kufanyabiashara; Tutaepuka kushirikiana na makampuni ambayo yanakiuka maadili ya kibiashara; Tutaunga mkono uanzishaji wa programu za kuzuia na kupambana na rushwa na kushiriki katika kutumia nyenzo na mikakati iliyoanzishwa kwa lengo la kuhakikisha uwepo wa uwazi, ufanisi na uadilifu katika shughuli za biashara; Tutaunga mkono kampeni za mapambano dhidi ya rushwa duniani kote ambazo zinadumisha mazingira ya haki katika soko na kuimarisha Utawala Bora na uwazi katika shughuli zote za biashara. Hatutatoa, kuwezesha, kushawishi au kutoa zawadi kwa Afisa yeyote wa Umma, familia zao au washirika wao wa kikazi katika shughuli inayohusiana na mchakato wa manunuzi au katika utekelezaji wa mkataba; Tamko: Ninakiri kuwa nimesoma masharti yaliyomo katika Hati hii ya Ahadi ya Uadilifu na kuyaelewa kabla ya kuweka sahihi. Ninakubaliana na kutambua kwamba masharti yaliyomo katika Hati hii ni ya kisheria na ya kimaadili na ninawajibika kuyafuata. Pia, ninafahamu kuwa ukiukwaji wa masharti hayo ni uvunjaji wa Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa, Sheria ya Ununuzi wa Umma, Sheria ya Uhujumu Uchumi au Sheria nyengine za nchi na hatua za kisheria zinaweza kuchukuliwa dhidi yangu iwapo nitakiuka masharti hayo. ………………………………. ……………… …....………. …………….. JINA LA MTENDAJI MKUU KAMPUNI SAINI TAREHE Muhuri wa Kampuni ……………… ………………………… …………………… …………….. JINA LA MTENDAJI MKUU -BRELA SAINI TAREHE 10. 11. 12. 13. 14.