WAZEE MAARUFU WATEMBELEA SHUGHULI ZA UTALII BWAWA LA LIHOGOSA, WANGING’OMBE.
Tarehe iliyowekwa: December 14th, 2025
WAZEE Maarufu wa wilaya ya Wanging’ombe wakiambatana na CHifu Mkoa wa Njombe, Bw. Charles Mkongwa wamefanya ziara na kutembelea shughuli za utalii katika Bwawa la Lihogosa lililopo kata ya Igima wilayani Wanging’ombe.
Akizungumza na Uongozi wa Kijiji cha Mawindi na wenyeji wa eneo hilo, Chifu wa Mkoa wa Njombe, Bw. Charles Mkongwa ametumia fursa hiyo kuombea chombo cha usafiri (fiber boat) na ujenzi wa gati kwa ajili ya shughuli za hapo bwawani pia amewataka wenyeji wa eneo hilo kuchangamkia fursa mbalimbali zitakazojitokeza eneo hilo kwa ajili ya kutoa huduma kwa wageni.