WANANCHI MKOANI NJOMBE WAMETAKIWA KUDUMISHA AMANI KWA MAENDELEO YA KIUCHUMI.
Tarehe iliyowekwa: November 6th, 2025
Na. Mwandishi Wetu,
Njombe RS,
RAI hiyo imetolewa Novemba 06,2025 na Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Mhe. Anthony Mtaka akiwa Katika Halmashauri ya Mji wa Makambako katika mkutano wa hadhara na Wafanyabishara pamoja na Wananchi.
Akizungumza katika hadhara hiyo Mhe. Mtaka amewasisitiza Wananchi kuhakikisha wanaripoti taarifa zote za viashiria vya uvunjifu wa amani.
“Ushirikiano baina ya jamii na vyombo vya ulinzi na usalama utaendelea kuimarisha usalama katika mji wetu wa Makambako kwani hakuna taarifa ya uvunjifu wa amani haitopuuzwa”, alisema Mhe. Mtaka.
Aidha, Mhe. Mtaka aliongeza kusema adhima ya Serikali ni kuhakikisha mji wa Makambako unakua zaidi kiuchumi huku akiwasisitiza Wananchi na Wafanyabiashara kuepuka vitendo vinavyosababisha machafuko.